Tetesi: Eti hatuko naye tena?

hata kama ni evidence hio ni circumstancial!:shut-mouth:
 
Huu ni mtazamo tu si halisia, na kwa mtazamo huu unaona yule dada ndio kasababisha au yule baba amesababisha huyo mama asababishe?
Una uhakika gani kwamba sio hali halisi??Nilivyomwelewa Michelle anasema kwamba kuna uwezekano na umuhimu wa kuangalia swala zima kwa undani zaidi na sio kwamba anasema kwa uhakika imetokea!Kusema sio hali halisi ina maana kwamba una uhakika...je nini kinakupa uhakika huo?
 
Tunaridhika kirahisi sana dearest...inaweza kua ni uvivu wa kuchimba na kuchambua mambo!
Mganga siku zote hajigangi Lizz no matter how intelligent she/he is. utachimba na kuchimbua at the end of the day hata unachokitafuta shimoni hukioni unafukia mashimo unaanza upya
 
Huu ni mtazamo tu si halisia, na kwa mtazamo huu unaona yule dada ndio kasababisha au yule baba amesababisha huyo mama asababishe?

ha ha ha ha ha....najua ni ngumu kunielewa....unapotaka kutoa hukumu unaangalia mazingira ya kitu,yanaweza yakawa si uhalisia lakini kama mazingira hata kama si uhalisia yanaweza kufanya yule/wale wanaotoa hukumu kutoa hukumu kwa kile wao wanachoona ndo uhalisia japo si uhalisia....uhalisia mi na wewe hatuujui ila naweza shinda kesi kwa kutengeneza uhalisia kuwa aliua na kama piaingewezekana kufanya autopsy kama alivyosema Lizzy ambapo ingewezekana ikakutwa sumu amabyo si lazima awe kaiweka huyo mama but kwa kupitia matukio ya nyuma na maneno ya kinywa chake huyo mama na ya mashahidi kama wewe mnayekiri alishauriwa vibaya kwenye lile tukio la kufumania...kwanini kama unakiri alishauriwa vibaya hapo nyuma akakubali, isiwezekane yeye kushauriwa vibaya kuua ukizingatia maneno yako alishafanya kila kitu kikashindikana mtu kutulia akawa na hasira mbaya....???
 
Na wewe Lizzy hujanielewa mimi sio nashabikia hapa tunajadili tu, uhalisia nimekubali hizo quote na majibu yake hayana uhalisia wowote ni mitazamo yangu na yake. Inaonekana mnamtetea mwanaume sasa mwanaume kama kafanyiziwa na mkewe nani aliyesababisha yote hayo?? hapo ndio swali? mahakamani hakuna aliyeachiwa huru kwa kitendo alichofanya bila kukusudia?
 
What it do mamito?
 
Hiyo si mpaka Dr athibitishe kwamba ugonjwa wa ini ulisababishwa na nini? Nakubali hasira yaweza kukufanya ufanye jambo baya, ila sio kwenye case hii, maradhi yake ndio yalimuua
 

baba yako akimuua mama yako kwa kuwa mama yako ali cheat akakuzaa wewe unataka tuone baba yako hana kosa kwasababu mama yako ndo alisababisha baba yako achukie na kupelekea kufanya vile? kwanini ajichukulie sheria mkononi?si angeweza ampatie divorce au kutengana au kumuadhibu vingine?? nimetoa mfano.....sina sababu yeyote ya kumtetea mwanaume, hapa tunajadiki mazingira ya kifo cha huyo baba.....

Mahakamani wapo wanaoachiwa kwa kuua bila kukusudia ila si kwa namna hii ya kuua....ni ile kama mtu ameua akijilinda...yaani pengine asimgemuua angekufa yeye kwa hiyo akamuwahi...huyu mama pia hatuna taarifa kuwa ana matatizo ya akili.....
 
hii discussion ilianza vizuri,ila naona mmepoteza muelekeo huku mwishoni,kama mmemaliza points si muiache tu hi thread irest in peace mnh...:fear:
 
Kwa hiyo angeweza kumuua wakati anamvunja mkono kwa mikono yake?kama ni kujitetea? angeweza kujitetea kwa kusema kaingiliwa na mwizi mpaka chumbani kwake?
 

mfano: baba yako akimuua mama yako kwa kuwa mama yako alitoka nje ya ndoa akakuzaa wewe,baba yako alikasirika kwasababu hiyo akamuua mama yako...kwa kuwa mama yako ndo alisababisha basi tumuache baba yako aendelee na maisha ye hana kosa? tungeishi hapa duniani kweli?kwanini aue? si angeweza mpa talaka au kutengana nae na kadhalika???? mwizi akiiba in a process akaua na huyo mwizi ni maskini au mama yake yu mautihuti tumuache kwasababu alikuwa na sababu nzuri ya kuua?

Watu wanaachiwa kama ilikuwa wasingeua wangeuawa wao...unafahamu circimstance kama hizo nafikiri.....au mtu ni kichaa....sasa kwa zase ya huyu mama ungesema nini?
 
hii discussion ilianza vizuri,ila naona mmepoteza muelekeo huku mwishoni,kama mmemaliza points si muiache tu hi thread irest in peace mnh...:fear:
Kweli kabisa, Ngoja niishie hapa Ukweli ni Mungu anajua na wenyewe, Michelle thanks kwa some law quotes, again, RIP Marehemu
 
Kwa hiyo angeweza kumuua wakati anamvunja mkono kwa mikono yake?kama ni kujitetea? angeweza kujitetea kwa kusema kaingiliwa na mwizi mpaka chumbani kwake?

ha ha ha ha ha.....umesema kafa kwa ugonjwa wa Ini na alikuwa nao muda;

huyu baba yawezekana kabisa kutokana na huyu mama alikuwa hawezi kupigana nae au kumuua kwa mikono yake akaamua kutumia njia nyingine ya kumuua taratibu au pia huu waweza kuwa uongo kwakuwa huyu baba kutokana na ugonjwa asingeweza kumpiga mkewe kwa namna ambayo ingembidi huyu mama aue ili yeye asife...mwanamke anatengeneza mazingira ya ku justify matendo yake...
 
Kweli kabisa, Ngoja niishie hapa Ukweli ni Mungu anajua na wenyewe, Michelle thanks kwa some law quotes, again, RIP Marehemu

Poa Gaga...ukweli ajua Mungu....pumzika kwa amani Magid!
 

Umenielewa sahihi Lizzy....kuelewa ni ngumu kwa baadhi...hakuna niliposema ameua ila kuna uwezekano....
 
Hiyo si mpaka Dr athibitishe kwamba ugonjwa wa ini ulisababishwa na nini? Nakubali hasira yaweza kukufanya ufanye jambo baya, ila sio kwenye case hii, maradhi yake ndio yalimuua

lazima Dr athibitishe....lets say Dr kathibitisha kweli kulikuwa na sumu...je ni nini kingetufanya tuamini kuwa ni huyu mama alimuwekea na si mtu mwingine??? hapo ndo inabidi tu connect dots....na dots zinazokuwa connected kirahisi ndo hizi japo yawezekana kabisa hiyo sumu hakupewa na mkewe labda aliwekewa kazini au bar na mtu ambaye alikuwa na bifu nae au mama alikuwa na mwanaume mwingine mzee akawa anaweka kiwingu....tunachojadili ni matukio kabla ya kifo na mazingira ya kifo....😛layball:
 
The great thinker very intelligent women wamekutana, haya msichanganye na depression na appretn na stress za ulonelyness. nawapenda nyote
Very constructive argument.
 
Michelle naomba uwe mwanasheria wangu kuna kesi flani ninayo mahali inahusu nyumba ndogo.....:A S shade:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…