Tetesi huanza na minong'ono

Tetesi huanza na minong'ono

Haya maisha tutendeane mema na kuombeana dua njema. Tukumbuke maneno haya:

Lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.

Mwisho wa siku kila mtu atalamba sakafu.
 
Tetesi huanza na minong'ono.. Hiyo minong'ono ikikoma huwa tetesi na tetesi zikikoma huwa breaking news..!
Dunia ya sasa iko uchi kutokana na maendeleo makubwa ya teknolojia.. Dunia haina siri tena!
Unafanya jambo gizani.. Tena giza totoro kabisa lakini unakuja kushangaa jambo hilo linakuja kuwekwa upenuni peupe kwa picha safi kabisa

Kuficha taarifa yoyote kubwa inayoihusu Jamii haisaidii chochote.. Tunaweza kafanya hivyo kwa lengo maalum na sababu maalum lakini kwa dunia hii ya sasa.. Taarifa zinaweza kuvuja zenyewe bila hata kuvujishwa na yoyote yule

Kuna madhara makubwa kwenye taarifa kuvuja zenyewe.. Maana ni sawa na bomba la maji lililopasuka na kuvujisha maji barabarani.. Yale maji hayana mwenyewe.. Yeyote anaweza kuyatumia vyovyote
Taarifa zinazovuja zenyewe hurembwa, hutiwa nakshi na kuongezewa vikolombwezo vya kila aina kulingana na mahitaji ya mlengwa!

Hakuna siri ya mtu moja duniani.. Ni fikra finyu kuruhusu minong'ono itawale kuliko kuweka wazi.. Akili ya binadamu ni kitu kisichozuilika.. Ukiibania taarifa unaiongezea udadisi na mshawasha wa kutaka kujua zaidi.. Kujua kulikoni...

Minong'ono ya Msechu kujiandaa kuingia studio ni uzushi usiofaa kupewa kipaza sauti
Mwafrika ubongo wake haujapevuka kiasi cha kujitawala. Fact. Hatujifunzi?
 
Back
Top Bottom