Wanabodi,
Declaration of interest.
Kwa vile mimi ni kada wa Chama Cha Mapinduzi, CCM na niligombea ubunge wa jimbo la Kawe, na Wajumbe wakafanya yao, naomba bandiko hili lisichukuliwe kama fursa ya mimi kumchafua Gwajiboy ili atemwe, nigombee tena!. Naomba ku declare my interest, sina mpango wowote kugombea ubunge wa Kawe hata bure, Wajumbe walichonifanya ile 2020, kimenitosha, sitathubutu tena kujaribu.
Kuhusu Tetesi
Ni habari unazozisikia juu juu sio kutoka any reliable source.
Kwa msio fahamu, mimi na kampuni yangu ya PPR ni wahanga wa mdororo wa uchumi uliosababishwa na Covid 19. Hivyo nililazimika kuuza magari yote, na sasa usafiri wangu ni TZ 11, Boda Boda, Dala Dala na mara moja moja Uber na Bolti.
Leo nikaita Bolt fulani, kumbe ni bolt ya kada. Kada akaona jina langu, hivyo nilipoingia tuu ndani ya gari, dereva akanisalimia kwa kunichangamkia, na kuniuliza, vipi haujaribu tena?, jimbo limeisha tangazwa kichini chini liko wazi!. Askofu Gwajima amemwagwa rasmi, ila haijatangazwa rasmi!.
Mtoaji habari wangu akasema Salama pekee ya Askofu Gwajima kuendelea na ubunge wake wa Kawe ni kujitokeza kuchanjwa hadharani, vinginevyo, it's a gone case!.
"Hivyo kama bado uko interested na Kawe jimbo liko wazi wewe tuu!.
Nilimweleza ukweli wangu, I'm not interested!.
My Take.
Kama tetesi hii ni kweli, Askofu Gwajima kosa lake ni lipi?.
Kama ni msimamo wake kupinga chanjo ya Corona, kwa vile chanjo ni hiyari, wanao support Chanjo waeleze umuhimu wa chanjo.
Ila pia wapinga chanjo with facts, waruhusiwe kuipinga kwa facts na wasikilizwe.
Gwajima avuliwe ubunge kwa kosa lipi?. Hii tetesi itakuwa ni uongo tuu ila pia with Chama changu CCM, mambo ya fitna, majungu na zengwe, anything is possible!.
Lets wait and see.
Paskali