Duh! Haya makubwa. Ina maana jamaa anajiandaa kutawala kwa mabavu wakati wapiga kura wengi zaidi watamkataa Oktoba 31?
Kuna wakati mwingine mimi huwa nashangaa kweli. Hivi kweli nyie watu wa CHADEMA seriously mnadhani kuwa SLAA atashinda? JK atashinda kwa kati ya ASILIMIA 77 NA 87 ya kura zitakazopigwa. Huu ndio ukweli. Maneno ya mitaani tuachane nayo. JK atashinda na CCM kwa ujumla itashinda sio kwa wizi wa kura bali kwa kukubaliwa na wananchi. SLAA atapata below 20% akifuatiwa na Prof. Lipumba. Sasa nyie wenye ndoto za SLAA kutwaa urais kaeni hivyo hivyo na muendelee na ndoto hizo. Mabadiliko hayaji kwa porojo na matumaini. Mabadiliko yatakuja kwa upinzani kufanya kazi na upinzani wenyewe ubadilike katika mbinu na mikakati. Mkiendelea na kauli za kumwaga damu, IKULU kamwe hamtaiona. Mkiendelea kuvaa magwanda yanu ya khaki na yenye sura ya kijeshi lile jengo jeupe mtalisikia kwenye bomba mpaka milelel.
Upinzani wa kweli katika nchi hii utatoka ndani ya CCM kama Nyerere alivyowahi kusema. Upinzani wa kweli hauwezi kutoka kwa wapiga porojo na wenye uchu wa madaraka na wasiojua hata kuichambua jamii waliyo nayo.