Kama Nchimbi anataka asiwe mhusika katika maovu haya yote, hana sababu yoyote ya kujiweka karibu na ushetani wa Samia Suluhu Hassan na Genge lake.
Kule kukubali tu kuwa mgombea mwenza katika taratibu mbovu namna ile kulimweka katika hali ngumu sana.
Anachoweza kufanya kujisafisha ni kuondoka moja kwa moja, siyo kubaki kimya tu. Watu watamchukulia kuwa anasubiri kutulie ili waovu waendeleze uovu wao.
Hawa wote, akina Mwigulu, Kabuti na wengine wote wanaouwezesha utawala feki uendelee kuwa madarakani, wote ni wachangiaji katika uovu dhidi ya waTanzania; na siku yao ikifika waamuliwe kwa uovu wao waliochangia kuwaumiza waTanzania.