Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 12,826
- 17,371
Ona huyu naye!Uongozi ni wito wa kuongoza wengine . uongozi sio ajira...
Kama huna uwezo wa kuongoza wengine basi huna haki ya kulazimisha upewe hiyo nafasi...
Tanzania kuna masikini Wengi wanachaguliwa Kwa uwezo wako...
Wala hakuna sababu ya kulialia upewe nafasi
Inamaana, Rais pamoja na Baraza lake la mawaziri, Wabunge, Rc's, Dc's nk nk, hawana ajira wanajitolea!
Nini maana ya ajira kwa tafsiri yako?
Na je teuzi hizi kiuhalisia zinafuata sifa za uongozi?
Wanakuwa wamesomea vyuo gani vya uongozi hao?
Umenikumbusha maswali ya kwenye usaili kipindi tunatafuta kazi!
Unaulizwa: "ni nini lengo la kutafuta kazi hii?"
Tulikaririshwa jibu eti..." kwenda kuitumikia nchi yangu".
Hakuna aliyekuwa akijibu: " kuajiriwa ili nipate pesa ya mshahara niweze kujikimu na maisha" ambao huo ndiyo ukweli, lakini hakuna aliyeusema!
Ndiyo wewe hapo eti "uongozi siyo ajira".
Labda unaongelea uongozi wa familia yako binafsi, lakini si kwa nafasi za uongozi wa kwenye vyama ama Serikalini, hizo ni ajira lengo ni mishahara.