Teuzi mbalimbali kujaa majina ya watoto wa viongozi na vigogo Serikalini kama taifa tunaelekea wapi?

Uongozi ni wito wa kuongoza wengine . uongozi sio ajira...
Kama huna uwezo wa kuongoza wengine basi huna haki ya kulazimisha upewe hiyo nafasi...
Tanzania kuna masikini Wengi wanachaguliwa Kwa uwezo wako...
Wala hakuna sababu ya kulialia upewe nafasi
Ona huyu naye!

Inamaana, Rais pamoja na Baraza lake la mawaziri, Wabunge, Rc's, Dc's nk nk, hawana ajira wanajitolea!

Nini maana ya ajira kwa tafsiri yako?

Na je teuzi hizi kiuhalisia zinafuata sifa za uongozi?

Wanakuwa wamesomea vyuo gani vya uongozi hao?

Umenikumbusha maswali ya kwenye usaili kipindi tunatafuta kazi!

Unaulizwa: "ni nini lengo la kutafuta kazi hii?"

Tulikaririshwa jibu eti..." kwenda kuitumikia nchi yangu".

Hakuna aliyekuwa akijibu: " kuajiriwa ili nipate pesa ya mshahara niweze kujikimu na maisha" ambao huo ndiyo ukweli, lakini hakuna aliyeusema!

Ndiyo wewe hapo eti "uongozi siyo ajira".

Labda unaongelea uongozi wa familia yako binafsi, lakini si kwa nafasi za uongozi wa kwenye vyama ama Serikalini, hizo ni ajira lengo ni mishahara.
 
Maskini ndio mnaowaweka hao wahuni na mnawapigia kura kila siku, tukiwaambia katiba mpya ambayo itakuwa na check and balance mnatutukana na kutuita hatuna akili, tunaotaka katiba mpya na hatutaki nafasi yeyote na tuko vizuri, tunataka Taifa bora lenye haki na usawa, jaribuni kutusikiliza hao wengine hawana jipya
 
Nilikuwa nawaza kuwa baada ya kipindi cha miaka 20 ijayo kutakuwa hakuna nafasi kwenye baraza la mawaziri, naibu, katibu, naibu katibu, wakuu wa mikoa na wilaya na mabalozi. Nafasi zitakuwa "zimesharithishwa" kwa wenyewe. Sie tujitahidi kujiajiri tu.
 
Anayeteua anajua sababu
 
Hii ni indicator mbaya ktk taswira ya Utaifa na ulinzi na usalama wa Taifa. Hili sio Taifa lakifalme why watu wanakalia viti wakitoka wanawarithisha watoto wao mbaya hawana uwezo wakuongoza. Hii ni hatari kwa Taifa. Time Will Make a way to show us the truth
 
Nilikuwa nawaza kuwa baada ya kipindi cha miaka 20 ijayo kutakuwa hakuna nafasi kwenye baraza la mawaziri, naibu, katibu, naibu katibu, wakuu wa mikoa na wilaya na mabalozi. Nafasi zitakuwa "zimesharithishwa" kwa wenyewe. Sie tujitahidi kujiajiri tu.

Unaposema ukajiajiri je hizo fursa ni nani anayeziandalia njia hili uweze kuziona na kuzitumia kama siyo hiyo hiyo serikali corrupt ndiyo unaitegemea kama mfanyabiashara iwe mtengenezaji wa sera nzuri, itoe usimamizi, i-support upatikanaji wa mitaji, ulinzi na mazingira rafiki kwa ajili ya hizo biashara kustawi na hatimaye kuwainua watu wake.
 

Wanasema muda ni tiba lakini tamaa ni kansa umkumba mtu yeyote yule atakayeonja utamu wa madaraka na mali.

Kitu pekee kinachoaminika kudhibiti tamaa ya binadamu kwa kiasi fulani ni kuwekewa kizingiti cha sheria na utaratibu wa kufuatwa.

Huku sheria ni msumeno ikiambatana na nguvu ya msukumo wa umma wote katika kuhakikisha hilo linatimizwa kwa vitendo na jamii nzima kila mmoja akiwajibika na kuwajibishwa kwa nafasi yake.
 
Current affairs hizi mkuu huwezi kosa kujua.

Kila mtu mwenye ndevu ama matiti kifuani anaelewa mambo yanavyokwenda nchini mwake, siyo mpaka utajiwe majina!
Damn wrong
Ktk nchi ambazo wananchi wake wana low political participation ni Tanzania πŸ‡ΉπŸ‡Ώ (Walitufundisha chuo kikuu)

Kwahiyo usiassume kila mtu anajua wengi wameachana na siasa moja ya sababu ni kuikatia tamaa ccm
Na kinacho tugonganisha mawazo hapa ni ushabiki na mahaba niue kwa upande mtu anakokuona ndiyo sahihi kwake ama anakonufaika nako.
Wrong again
Mtu angekuwa keshatetea kuwa mtoa mada kakosea bila ushahidi ndiyo ungesema ni ushahidi

Ila ninauliza alete ushahidi unasema ni mahabba?πŸ˜‚
Lakini kusema mpaka mtu akutajie ndiyo u prove, huo ni utani kama ulivyo utani mwingine tu.
Mkuu hapa sio kijiweni

Unaleta madai na ushahidi ku support madai yako

Unajua utani ni nini?

Utani ni kuleta madai bila ushahidi halafu ukataka tukusupport bila kuuliza

NB: ishu ni nyepesi jamaa angeenda twitter aka download mikeka ya teuzi then akaleta hapa, Simple.
 
Ahsante! Natamani sauti kama hizi zingepazwa na kuifikia umma nzima ya wabongo walalahoi walio wengi ingeamsha ari na kuchochea chachu ya mabadiliko .
 
Hakika!!
 
Mmeshafunga ambiwa bodaboda ni kazi
Ukweli hali ni ngumu kitaa na vibarua wanavyo wachache wengi wanataabika na njaa juani kutwa wakitafuta sumni ambayo nayo haipatikani mpaka kwa jasho la damu.
 
Kama hamna Mwanaukoo wako aliyekuwa na Elimu ya Chuo Kikuu kabla ya Kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977 basi vumulia tu kama wengine maana AWALI NI AWALI TU na hamnaga AWALI MBOVU...

Wakati wengine wanakomaa na UMANDE wengine walikuwa wanacheza Ngoma za Asili πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 

Kwahiyo ni mwendo wa kuendelea na msoto na kurithisha u-jobless kizazi kimoja mpaka kingine.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…