Jambo la ajabu ni kuwa, japo Mama amemwona Makonda kuwa ni hatari kwa chama, lakini hajaweza kuachana naye kabisa. Afrika tuna safari ndefu kwa mambo haya ya teuzi zisizozingatia weledi na sifa stahiki.
Paul Makonda ni wale watu Waingereza wanawaita controversial figures, watu wenye mtafaruku. Hawa hawaeleweki na wakati mwingine ni opportunistic, watu wanaotumia fursa zinazojitokeza kujipatia umaarufu binafsi. Watu kama akina Makonda ni populists, tena self-centered populists, hawa watu huangalia umaarufu wao tu na jinsi umma unavyowaona. Mahali pengine wanaweza kuwa divisive, yaani ni watu ambao huwagawa watu kwa matendo yao na kuiacha jamii ikigawanyika huku na huko.
Makonda hajawahi kusimama kwa manufaa ya umma pasipo kujiweka yeye mwenyewe mbele ya maslahi ya umma. Hawa akina Makonda ni king makers, ni washenga, lakini wanaweza kuwa hatari kwa hao kings kwani kuwageuka mabosi wao ni dakika tu sifuri tu, kwani wanaujua unafiki vizuri. Watu kama akina Makonda hutumika kama curtains au hata cartels pia, hutumika kama pazia na vikaragosi ambapo nyuma yako hujificha wakubwa na kufanya watakayo.
Mwisho wa watu kama akina Makonda ni kwa Taifa kupoteza, vyama kupoteza, viongozi kupoteza na vibaraka hawa nao kupoteza. Kwa ujumja watu kama akina Makonda hutumika katika siasa za kihalifu. Hawa mifano yake ni akina Sabaya, na mnajua mwisho Taifa lilipoteza, CCM ilipoteza, Magufuli alipoteza na Sabaya naye alipoteza.