Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 60
Toa mapendekezo sasa, sio kupinga tu.
Nurujamii,
Ulishaambiwa hapa JF hakuna anayependelewa na ndio maana wale wanaopondea JF kila mara kuwa ni kijiwe cha CHADEMA walichemsha maana hapa kila mtu hata kina Mnyika hupata dosier yao.
Issue hapa ni tahadhari hata kwa huyo Zitto kama akikubali huo uteuzi wa Kikwete kujua kuwa hakuna ize ride hapa. Akikubaliana na ushenzi na spin za kina Mwakyembe na Mark Bomani atapata the same standard toka kwa JF members.
So far, issue ya kumweka Mwakyembe na Mark Bomani kwenye hii kamati ni ushahidi tosha kuwa usanii unatumika hapa. Hii kamati imepewa onyo na wanaJF kuwa watanzania hawataki usanii kwa hiyo kila kinachosemwa hapa ni muhimu!
Wana JF nadhani tufike mahali tutumie Busara. Tukitaka kila mtu awepo kwenye kamati basi kutakuwa na watu wengi saaana. Ikumbukwe kwamba hii kamati
itatumia pesa za walipa kodi kuweza kutekeleza majukumu yake watu wakiwa wengi peas zaidi.
ikumbukwe kwamba hii kamati haitakaa ndani ya chupa kujifungia huko wakati inafanya kazi yake. Itahitaji ushauri wa kitaalum kutoka kwa watu wengine pale inapobidi kufanya hivyo
Hivyo basi badala ya kuanza kuponda kama huu ni wakati wa kuwapa inputs ili wanapifanya mchakato huo wajue ni vitu gani vimekosekana viongezwe, vipunguzwe, n.k
Nawakilisha hoja
Wazee naomba kuuliza swali tu Hivi Hadidu za Rejea maana yake nini maana mmeniacha kabisa na sielewi maana yake. Tafadhalini.
..
Hivi Zitto alipofukuzwa bungeni mlitaka JK aingilie kati na kumrudisha. Nini maana ya nguzo tatu za mamlaka ya nchi?
....
Mwafrika wa Kike,
Naona hata angewekwa Yesu kwenye hiyo kamati bado ungelalamika. Ungesema mbona hakuwekwa Mtume?
Hii ni hatua nzuri na inabidi kuipongeza. Kuwepo kwa Dr. Mwakyembe kuna matatizo gani? Pamoja na matatizo yake lakini Mwakyembe ana uwezo. Alipokuwa anatetea NMB mbona watu wote walikuwa wanamshangilia? Au Bomani ana matatizo gani mbona useme hivyo?
Lazima ifike mahali tuache kulalamika. Kinachotakiwa sasa ni kuwatumia watu kama akina Zitto ili kuwapa mawazo na maoni yetu kwa faida ya nchi yetu.
Hapo anajaribu kuwa smart.Kama kweli JK ana nia ya dhati mi nampa tano.Kumbe Jk alimuona Zitto alikua na point ila sasa mheshimiwa rais uwaambie hao manazi waliomshupalia Zitto bungeni next time wajaribu kuweka maslahi ya taifa mbele.
Lakini kama anaweka usanii itamcost kuliko anavyotegemea.
Hapo nakufagilia mzee,
Hili la kumuweka Cheyo lina utata sana.Kwanini iwe Cheyo kwani hapo mimi naona kama mbunge wa upinzani yupo mmoja tu.Nadhani pia Jk kumweka cheyo hiyo ni strategy fulani fishy anataka kuachieve.
Hebu ngoja tumpe cheyo muda tutamsikia
Hadidu Rejea ni Terms of Reference
JK anacheza tu kuendelea kufuja pesa ya walipa kodi. Tumechoka na alinacha, hizi kamati uchwara ambazo brief yake inakuwa haijitoshelezeki (au siri) na kisha yeye kupewa report na kuiweka kwenye makabati na kuozea huko magogoni.
Hivi ni kitu gani kigumu kwa rais kuchukua uamuzi wa kusitisha mikataba yote mibovu with immediate effect na kuwa na mpango mpya kwa wale wanaopenda na wale wasiopenda watupeleke mahakamani kutafuta haki yao. Hatupati faida kabisa na haya mazingaombwe.
Mwaka jana wakati tunapiga kelele za Richimondulian walisema ni kelele za mlango leo hii wanaunda kamati tena nje ya bunge ambalo ndio lilikuwa sahihi kufanya mambo kama haya, kulikoni? JK na usanii wake hawezi kufanikiwa hadi pale atakapoacha kubeza na kuangalia maslahi ya Tanzania. Mafisadi wamejaa tele tena bila aibu wanaendelea kula kama vile pesa ya walipa kodi iliwekwa alama walipozaliwa kwamba ni ya kwao. Sasa rais ameshindwa kuwawajibisha Karamagi et al ataweza kwenye hili la mikataba? Ataweza kuchukua hatua wakati anafahamu fika pesa ilivyoliwa na kutafunwa na wajanja kutoka BOT?
Haya ni yale ambayo sisi ambao hatuna wafanyakazi wa ziada wa kutuletea maswala (habari) mbali mbali, vipi yeye ambaye usalama wa taifa wanampelekea habari kila uchwao kuhusu nini kinaendelea? Wakati huo huo wanalipwa na pesa ya walipa kodi. JK ACHA KAMBA, WASHIKISHE ADABU MAFISADI NA FUTA MIKATABA YOTE MIBOVU NDIO MAANA YA KUWA RAIS KUCHUKUA MAAMUZI MAGUMU.
mwafrika, kusema ukweli tangu JK aingie madarakani jambo hili alilofanya leo limenifurahisha sana,. nakubali kwamba anayo matatizo na mapungufu mengi sana, lakini i think it's very convinient to appreciate what he does and praise him.
Hivi Zitto alipofukuzwa bungeni mlitaka JK aingilie kati na kumrudisha. Nini maana ya nguzo tatu za mamlaka ya nchi?
This is the more than kamati. It is a strong message to Spika and the wabunge kwamba what they did (to expel Zitto) was wrong.
Ulichofanya hapa ndio kinatakiwa pia, wewe sifia na kutoa mapendekezo yako at the same time ukiwaruhusu pia wale wengine wanaotaka kupondea kufanya hivyo.
Kumponda aliunda kamati bado haisaidii maana haibadilishi chochote pia kusifia hiyo kamati bado hailet mabadaliko. kitakacholeta mabadiliko ni utendaji wa kama yenyewe na wanaJF kumbuka wanaJF tunaweza kuwa part ya hii kamati indirectly.
Otherwise natoa wito wa watu wanaopinga mtu fulani kwenye hiyo kamati walau atoe sababu 3 hadi 5 za kumpinga
Nawakilisha
usanii mtupu katika hiyo kamati..
natoa wasifu mdogo wa watu waliochaguliwa katika kamati hiyo,kesho ntamwaga zaidi..
bwana MACHUNDE,ni mwajiriliwa wa kampuni ya karamagi inaitwa tradex Investment.wametaja soko la hisa ili kuwahadaa watz,
bwana maige si mwanasheria na hana uzoefu wowote ktk sekta ya madini,ni Rafiki mkubwa wa mh. ngeleja<naibu waziri-madini>.
bwana cheyo,toka arudushiwe nyumba yake amekuwa kada invisible wa sisiemu,
itaendelea..
Kamati au tume au whatever the heck waliita iliyokuwa inapitia mikataba ya madini wakati wa Buzwagi ukisainiwa London ilikuwa na tofauti gani na hii kamati mbovu ya Bomani, Mwakyembe, na Cheyo?