Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Mojawapo ya mambo ambayo hawa waitwao ‘viongozi’ wetu wanayaweza ni kuteua na kutengua watu wa kuzijaza nafasi za uongozi hususan serikalini na kwenye idara zake.
Na jambo kubwa linalonichefua sana ni hii dhana ya kuonekana mtu ‘kaula’ anapoteuliwa na Rais kwenye nafasi yoyote ile ya kiuongozi.
Kuna nini cha ‘kula’ kwenye utumishi wa umma wa nchi iliyo maskini kama hii Tanzania yetu?
Kuwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya, na kadhalika, kuna nini cha ‘kula’ mpaka iwe shangwe kwa watu pale mtu mmoja anapoteuliwa kwenda kuitumikia hiyo nafasi?
Hayo yote ni matokeo ya udhaifu wa uongozi wa CCM.
Uongozi wa CCM umejenga utamaduni wa kinyumenyume kabisa.
Badala ya kwenda kuwatumikia wananchi, wateuliwa wa serikali za CCM huwa wanajinufaisha wao tu.
Sikumbuki kuona au kusikia popote pale Rais kutoka CCM aliyekemea hii dhana hasi ya ‘kuula’.
Marais wa CCM wanachokiweza ni kuteua na kutengua, hususan Rais Samia na mtangulizi wake.
Kutwa kucha kuteua tu lakini hawakemei dhana potofu ya ‘kuula’!
Rais mwepesi [lightweight]. Chama tawala ni chepesi. Umma [idadi kubwa] haujielewi.
Typical banana republic.