Teuzi zile zile, wateuliwa wale wale, kama haujawahi kuwemo hautakuwemo milele

Kuna watu wamezaliwa mchana wengine usiku wa Giza Totoro. Hivi ni kwanini teuzi zinazunguka kwa watu wale wale? Anatolewa huku anapelekwa kule, hata akistaafu anaambiwa tunakupa kazi ya kukusaidia kukushika mkono.

Inafikia mtu anazeeka anashindwa hata kuandika au kunyanyuka kwenye kiti bado ni mteuliwa. Kwanini hatutaki damu changa? Hawa vijana tunaowasomesha wataajaliwa na nani na wapi?? Teuzi za kujuana na Asante zitaisha lini?

Teuzi za baba yake au mama yake aliitumikia nchi lazima na yeye awemo zitaisha lini? Ikifika hatua ya teuzi mimi huwa napandwa na hasira. Mnawachukua wastaafu mnawaajiri tena. Koo zile zile, kabila zile zile na jamii ile ile.

Duuuu!!
Bora uteue unaowajua kuliko kuteua wasiojulikana..

Maisha ndivyo yalivyo mkuu huna connection utapiga miayo hadi unazeeka.
 
UKISTAAFU UNATEULIWA TENA
 
Kuwa mzalendo na ipende nchi yako, Tambua kuwa uongozi unatoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye anakufahamu wewe ukiwa bado katika tumbo la mama yako, Hivyo Kama mwenyezi Mungu alikupangia uwe kiongozi atakupatia nafasi ya kuwatumikia watu,

Lakini Kama mwenyezi Mungu hajawahi kukusudia wewe uwe kiongozi kuwatumikia watu, Basi Tambua kuwa hutakaa uwe kiongozi Bali utatumika na kutumikia eneo lingine kulingana na kipawa na kalama uliyo pewa na mwenyezi

mungu hawezi kukuinua uwe kiongozi wakati anajuwa huna wito wa uongozi, huna hekima,huna busara za uongozi,huna uvumilivu Wala Subira, huna kifua Cha kutunza Siri za kiuongozi kwa maslahi mapana ya Taifa letu, huna huruma Wala upendo kwa watu, huna moyo wa kujituma Wala kujishusha, Wala kuwa mnyenyekevu kwa watu, huwaheshimu watu waliokuzidi umri hata Kama umewazidi cheo

Hivyo uongozi Ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu na kwa wewe hufai kuwa kiongozi maana inaonyesha huna uvumilivu Wala Subira, Ni mlalamishi kana kwamba Ni Haki yako wewe kuwa kiongozi, ukipewa uongozi bila Shaka unaweza ukatuumiza sisi ambao siyo viongozi ili uendelee kubaki katika kiti cha uongozi, unaweza ukafanya Jambo lolote lile ilimradi tu ubaki kuwa kiongozi Kama fahari yako badala ya kuona Ni nafasi ya kuwatumikia watu

Uongozi Ni utumishi kwa watu Ila wewe mwenzangu na Mimi inaonyesha unauhitaji wa uongozi ili ujineemeshe mwenyewe, Ndio maana unaona wengine Ni Kama wanafaidi sana na hivyo ungependa nawewe upewe ili ujinufaishe mwenyewe
Hili gazeti lote, halijajibu hoja ya msingi. Acha kumsingizia Mungu kwakila kitu, halafu kiongozi akiharibu utamtaja Mungu tena au!!!!
 
Niliwahi kuandika humu ila ni ngumu kupata hiyo reply, kiufupi unatakiwa kupambana kuingia kwenye siasa kwa nguvu zako na vyovyote unavyoweza Mungu/Allah akiwa mbele, ukitoboa hapo basi hata wajukuu wanakuja kula njiani mwako.

Angalia mfano mtu kama burembo!.
 
Ndio maana huko Zanzibar takukuru hawajapeleka kesi hata moja mahakamani kwa kipindi cha mwaka mzima.

Mambo haya haya ya kulindana.

Tunafunika uoza.
 
Mfumo ndiyo unataka hivyo

Sasa mnataka nyie muingie na mlete

Na kufanya mapingamizi

Na muende tofauti na wao

Ova
Huo mfumo ulitengenezwa lini na aliuleta nani?? Yalikuepo hayo utumishi Magufuli akayabomoa kabisa ila kwenye uongozi naona bado. System ipi wakati nchi ni ya watanzania wote nanani anakidhi hivyo vigezo mpaka aingie kwenye hiyo system wakati kunawatu wanaelimu na maarifa makubwa kuzidi hao viongozi waliopo saizi.
 
Au na wewe umesikia jina Maua Daftari kama mimi?.
 
Bora uteue unaowajua kuliko kuteua wasiojulikana..

Maisha ndivyo yalivyo mkuu huna connection utapiga miayo hadi unazeeka.
Weka kwenye connection kwenye madili ila sio uongozi, utaua unachokiongoza mfano ni hii nchi yetu. Kuna watu wameongoza familia na koo zao tangu watoto kutokana na wazazi kutokuepo uje umfananishe na mtu ambaye yeye amezoea kila kitu kupewa bila jitihada ambao hao sasa ndio wanaconnection. Tutaangamiza taifa!
 
Kuwa mzalendo na ipende nchi yako, Tambua kuwa uongozi unatoka kwa Mwenyezi Mungu ambaye anakufahamu wewe ukiwa bado katika tumbo la mama yako, Hivyo Kama mwenyezi Mungu alikupangia uwe kiongozi atakupatia nafasi ya kuwatumikia watu,

Lakini Kama mwenyezi Mungu hajawahi kukusudia wewe uwe kiongozi kuwatumikia watu, Basi Tambua kuwa hutakaa uwe kiongozi Bali utatumika na kutumikia eneo lingine kulingana na kipawa na kalama uliyo pewa na mwenyezi

mungu hawezi kukuinua uwe kiongozi wakati anajuwa huna wito wa uongozi, huna hekima,huna busara za uongozi,huna uvumilivu Wala Subira, huna kifua Cha kutunza Siri za kiuongozi kwa maslahi mapana ya Taifa letu, huna huruma Wala upendo kwa watu, huna moyo wa kujituma Wala kujishusha, Wala kuwa mnyenyekevu kwa watu, huwaheshimu watu waliokuzidi umri hata Kama umewazidi cheo

Hivyo uongozi Ni majaliwa ya Mwenyezi Mungu na kwa wewe hufai kuwa kiongozi maana inaonyesha huna uvumilivu Wala Subira, Ni mlalamishi kana kwamba Ni Haki yako wewe kuwa kiongozi, ukipewa uongozi bila Shaka unaweza ukatuumiza sisi ambao siyo viongozi ili uendelee kubaki katika kiti cha uongozi, unaweza ukafanya Jambo lolote lile ilimradi tu ubaki kuwa kiongozi Kama fahari yako badala ya kuona Ni nafasi ya kuwatumikia watu

Uongozi Ni utumishi kwa watu Ila wewe mwenzangu na Mimi inaonyesha unauhitaji wa uongozi ili ujineemeshe mwenyewe, Ndio maana unaona wengine Ni Kama wanafaidi sana na hivyo ungependa nawewe upewe ili ujinufaishe mwenyewe
Unaandika mambo mengi halafu hakuna maana yoyote. Unamsingizia Mungu upumbafu wa wanadamu tu
 
Back
Top Bottom