Tevez Huyooooo!

Junius

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2009
Posts
3,181
Reaction score
144
Following contact received from Carlos Tevez’s advisors last night, in advance of the deadline the Club set for concluding negotiations, Manchester United announces that Carlos will not be signing a new contract with the Club.
The Club agreed to pay the option price of £25.5m and offered Carlos a five-year contract which would have made him one of its highest paid players.
Disappointingly however, his advisors informed the Club that, despite the success he has enjoyed during one of the Club’s most successful periods, he does not wish to continue playing for Manchester United.
The Club would like to thank Carlos for his services over the last two seasons and wishes him good luck for the future.

manutd.com
 
jamaa labda atatua chelsea manake man city wameshakubaliana kumchukua santa cruz.
 
Inaonesha yeye na watu wanaozunguka wana tamaa ya faranga kinyama. Ila akienda timu ovyoovyo atakuwa irrelevant muda si mrefu.
 
Inaonesha yeye na watu wanaozunguka wana tamaa ya faranga kinyama. Ila akienda timu ovyoovyo atakuwa irrelevant muda si mrefu.

Hapana Abdulhalim, Tevez alikuwa na hamu sana ya kubaki MANU kwa muda mrefu lakini kama kawaida ya SAF akawa haonyeshi kumthamini na mara nyingi kumweka benchi hadi plae alipokuwa desperate katika baadhi ya mechi ndiyo alipomuingiza. Jinsi alivyoisaidia MANU kuupata ushindi wa EPL 2009, SAF ilibidi amuonyeshe respect angalau kidogo lakini wapi. Baada ya Ronaldo kuamua kuondoka ndiyo SAF na management wakawa desperate kutaka kumbakisha. Mimi namuunga mkono Tevez kwamba kafanya uamuzi mzuri. Huyu SAF inabidi aanze kujifunza namna ya kuwaheshimu wachezaji wake hasa ambao mchango wao umeiletea mafanikio makubwa MANU.
 
swala lake ni kama la flamini anaona kama kawakomoa man united hapo.

Ishu ya Flamini nasikia iligomba eti pauni elfu 5 kwenye mshahara..kibabu Wenger kikakomaa hadi jamaa akajiondokea. Hata hivyo Flamini ameula wa chuya yeye na Hleb wake, wanabaki kulilia mto wakati daraja wameliunguza wenyewe.

Tevez nasikia alitaka alipwe mshahara mkubwa zaidi kuliko watu wote Man U pamoja na kwamba tayari anakamata pauni 90,000 kwa wiki. Wapambe wake nao ni nuksi ..kuna huyo muirani mwenye kukamata madocument yake naye anataka amalize shida zake zoote kwa kutumia mgongo wa Tevez..

Yetu macho tuone itakavyokuwa.
 

Mazee ktk klabu kubwa kama Man U hamna mchezaji aliye juu ya kocha na hiyo ndo principle ya SAF..ndo maana alimuuzilia mbali Beckham ingawa alikuwa kwenye peak na bado jahazi likasonga mbele..hio ndo tofauti ya SAF na mameneja wengine..yaani yeye hataki kuwa second kwa yeyote.

Technically mimi nimemsoma na kumuelewa kwa sababu sometimes alitaka kutumia formation ya striker mmoja..sasa hawezi kupangua fomesheni kumfurahisha Tevez. Pili lazima tuzingatie kuwa Tevez alikuwa kwa mkopo wakati ikumbukwe kuwa alimnunua Berba kwa club rekodi fee..sasa ingekuwa ajabu ampange Tevez zaidi wakati Berba ni mchezaji wa Man U na amenunuliwa kwa fedha nyingi kucheza. Nadhani Tevez alishaanza kujiona amepanda chati akasahau kuwa SAF hanaga masiara kwenye kazi yake.
 

Lakini ujue kwamba wachezaji wanaongea na katika kuongea sifa mbaya za SAF katika treatment ya wachezaji inazidi kufahamika zaidi baada ya muda utakuta wachezaji wazuri wengi wanakacha kusign na MANU, maana kuna mifano hai ya wachezaji ambao waliondoka kutokana na kutoridhika na treatment waliyoipata. List inazidi kuongezeka tu kwanza Beckham, Ronaldo, Tevez sijui ni yupi atakayefuata. Kwa jinsi nilivyomuona TEVES sidhani kama alijiona amepanda chart bali alitaka opportunity tu ya kucheza na kuisaidia timu kitu ambacho alikifanya katika mechi nyingi alizopewa nafasi. Hata mechi yake ya mwisho wapenzi walimpa standing O kwa jinsi walivyompenda na kumuona kwamba alikuwa mchezaji ambaye alicheza kwa uwezo wake wote alipokuwa uwanjani ili kuhakikisha ushindi.
 
Nilijua tu angeondoka, si wote tulimwona siku ile baada ya game ya gunners alivyokuwa akiwaaga mashabiki? Alishagundua kuwa no matter how hard angejituma au magoli angefunga- bado babu Fergie angempiga bench, na yeye anajijua kuwa sio mtu wa bench na alikuwa anahofu kwamba angeendelea kukaa pale ingeweza mcost nafasi yake kwenda Sauzi mwakani. Time to pull out your wallet Mr Wenger, show us some magic!
 

Here we go again lol! Hivi issue ya Tevez unaijua vizuri au unaongea kishabiki kama kawaida?
However, after declaring earlier this season he was deeply unhappy at a perceived lack of match action - even though he made more appearances than either Wayne Rooney or Dimitar Berbatov, it was always likely the South American would move on.
Kuna wachezaji kama akina Giggs, Scholes, Brown ,Neville wamekaa Man U maisha yao mengi ya uchezaji mpira hao nao utasemaje?
 
Tevez alikuwa ameshaanza kiburi na fergie ukishamuonyesha kiburi lazima akung'oe.
akiwa sub anajidai kushikilia beji ya manu na kuibusu huku washabiki wakimshangilia - kwa fergie ukifanya hivyo lazima akuong'oe
 
Tevez alikuwa ameshaanza kiburi na fergie ukishamuonyesha kiburi lazima akung'oe.
akiwa sub anajidai kushikilia beji ya manu na kuibusu huku washabiki wakimshangilia - kwa fergie ukifanya hivyo lazima akuong'oe

Tevez hajang'olewa, ameng'oka mwenyewe!
 
wacha waipate freshi walimnyanyasa vya kutosha,ameumizwa vya kutosha kisa wanatamani nafasi yake wawape rafiki zao wa ureno sasa sir alex fegi kiburi yake itamtokea puani mpaka leo na pesa zake hajui wa kumsajili hii itakuwa fundisho kati ya wachezaji anowataka hakuna anayefanana na teves ferdha kando na uwezo kando kila akigusa anapigwa dau karibu na ronaldo atajuuta kummfahamu teves ni hii itamjengea heshima kubwa kijana huyu wa argentina.
 

Humjui Furgerson wewe. Ni kocha pekee asiye na masihala katika usajili.
Mchezaji mzuri yeyote duniani anaweza kumsajili.
lakini ana vigezo kaviweka. NIDHAMU. Ukikosa hicho hata kama wewe ni mchezaji mzuri kiasi gani, benchi utalisugua na ushindi kwake is still obvious.
 

....inaelekea wewe ni mgeni kwenye soka........na hasa kwa huyu babu SAF......hivi unajua/unakumbuka Ronaldo aliendaje OT...........
 

Kuna wachezaji aliwataka na walikataa kwenda, mfano Ronaldhino na hivi karibuni Obi Mikel, sio kila mchezaji anataka kucheza @ Utd kama munavyotaka tuamini, kuna wachezaji hasa hawa wa South America hawataki kabisa kuishi huko Manchester especially kama wana watoto, ni mji mmoja boring sana na mvua haziishi kila siku, akina Veron, kleberson walishindwa kabisa ku-adapt na hata Ronaldo kuhama kwake imechangia kwa kiasi kikubwa na weather ya Manchester.
 

-Veron na Kleberson, style ya uchezaji wa England iliwashinda kuadopt. Kama kumbukumbu yako ni nzuri fuatilia mahojiano ya Fergie ya May 7 2002 alisema nini kuhusu Veron na isitoshe Veron hakutaka kwenda Chelsea alitaka kubaki Manchester "to fight for his place"

-Ronaldo, alishasema kuwa tangu utotoni dream yake ni kucheza Real Madrid, Kumbuka amekaa Manchester miaka sita, hiyo weather kumshinda imeanza season iliyopita au?

Sasa kama Manchester weather ni mbaya, mbona huyu Tevez anafikiria kwenda Man Cit au mvua huwa hainyeshi hapo Maine Road?
 
Last edited:
Mbona hujaelezea issue ya FLAMINI mkubwa?
Ukweli ni kwamba MAN U hawakutaka kumsajili TEVEZ tangu mwanzo na walishafanya uamuzi huo mapema wakaja kukumbuka shuka asubuhi
Popote atakapokwenda still atakumbukwa Old Trafford tunamtakia kila la heri
Naamini ataenda kwa jirani zetu Man City
 
Acha kutudanganya Ronaldinho aligoma kwenda Uingereza na alichagua Spain kwa sababu ya hali ya hewa na sio Ferguson Obi Mikel na Roben ilikuwa waje OT na aliyefanya mipango ni mzee wa FITINA PETER KENYON alivyochukuliwa na Abromovic akawashawishi wote wasiende Man United

Na Beckham,Ruud,Stam,Forlan nao walihama kwa sababu ya hali ya hewa?
Kitu kingine ni kuwa kila mchezaji anaisifia timuanayoichezea aukocha anamfundisha kwa wakati ule akishatoka anaanza kumkashifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…