Shida ni kwamba humu JF kila mtu anajifanya mjuaji hata kama hana alijualo. MKUU,ILA MIMI NILISHAKUELEWA SANA KWENYE ENEO LA SOKA..
Utasikia mwanaJF anasema "ushirikina na soka wapi na wapi"?, mara Oooh " usilete imani za kijinga hapa!" au "kama uchawi una msaada kwenye soka si Tanzania ingeshabeba World Cup, na timu za Sumbawanga zingekuwa zinatesa Ligi ya Mabingwa Afrika?" Basi mi nabaki nawaangalia tu.
Cha ajabu,jitu hilo hilo unakuta linatoka familia ya washirikina, mwanasiasa au mwanasoka mahiri linayemkubali ndo mshirikina no.1, bado yule Askofu,Mchungaji,Padre na Shehe wake. Mi huwa nayaangalia tu.