TFF, Bodi ya ligi, Simba na Yanga mna agenda Moja, mnatuona mashabiki malofa

TFF, Bodi ya ligi, Simba na Yanga mna agenda Moja, mnatuona mashabiki malofa

Atawaalika viongozi wa yanga na Simba ikulu kula nao, atatoa 200 million kwa kila mmoja kwa kigezo cha kulieshimisha taifa kimataifa then atawatangazia kuwa mgeni rasmi kweye derby
Mganga wangu kaniambia hivyo
 
Yaniiiii mtani niombeeeee 🤣 🤣 🤣 🤣 🤣 nilisema nitaingia tuu JF ila huku sport sikanyagi ila daaah hizi mada za derby zimekua nyingi na zinakeraaaa...kwa sbb nakuta notification 200 plus... ila naondoka kweli sirudi tena humu mpk Yesu afufuke..😊😊😊😊
🤣😃Nisikuone huku we kolo hadi Yesu afufuke tutakuwa tushachukua points 3 na makolo wameshuka daraja
 
Hawa watu wametengeneza mgogoro na wanajua njia ya kuhusuluhisha maofsini.

Nimeamini Simba na Yanga zinatumika kisiasa, na Toka Leo sitajisumbua na hizi timu

Wakiona derby isiharibu shughuli ya wanawake duniani, macho na masikio yawe Arusha badala ya Chang'ombe uwanja wa Taifa, maana aliyetarajiwa kuwa mgeni rasmi wa derby ndo alikuwa Arusha kwenye siku ya wanawake

Derby ya Kariakoo ni platform kubwa ya kisiasa ambapo hapa tupo siku za mwisho kuelekea uchaguzi mkuu mwezi Oktober, na kabla ya hapo Kuna uwezekano mkubwa derby nyingine ikawa halijatokea katika calendar
Mama kutoka jumba jeupe hataki kuipoteza hii fursa
Ilipigwa simu Moja tu derby ihairishwe na mama kutoka jumba jeupe awe mgeni rasmi kwenye derby na ipigwe tarehe rafiki ili awepo

Nina uhakika mechi ya marudiano ipo 💯 na mgeni rasmi atakuwa mtu mazito mno

1. Simba

Nilishangaa timu yenye uzoefu kama Simba igomee mechi kisa pitch feeling ya dakika 20 tu na wanajua itifaki na taratibu zote, pamoja na adhabu ya kukatwa points, kulipa faini ya million 5 na kushushwa daraja.
Kwa timu makini kama Simba hawawezi ku risk na kujiingiza katika hatari hii

2. Bodi ya ligi

Baada ya Simba kuandika barua ya kulalamikia minor ishu bodi ya ligi wakaitisha kikao na kamati ya masaa 72, yaani kamati ya masaa 72 inatathmini mchezo ambao haujafanyika🤣😅 hiki ni kichekesho.

Na bodi ya ligi ndo mtunga kanuni waamue kuvunja mechi Kwa sababu za kibwege tu. Na wanajua Yanga walienda CAS ni hujuma mbaya sana

3 Young Africans
Makamu wa Rais wa Yanga akaibuka na kauli ya msimamo hewa ati mechi haichezwi tena na sisi mashabiki tukadakia

Leo asbh kabla ya misa ya kwanza bus la Young Africans likaamukia Bunju kwenye uwanja wa Simba na mabango ya TUNAMSAKA MY WETU, hii ni kuonesha kuwa mechi ikipangiwa tarehe nyingine mashabiki wawe tayari akilini kuwa Simba walikimbia Sasa laZima wacheze ili wamfunge MY WETU

4. TFF
Ukimya wa taasisi ya football kidogo umenishangaza, hawajakemea Simba,Yanga wala bodi ya ligi, wao wapo kimya tu,

TFF hawajaomba radhi Kwa mashabiki na wawekezaji waliopata usumbufu kama Azam media

5 Wizara ya michezo na serika

Wizara ya michezo akina maana FA hawa ndo wanatembeaga na sandarusi la pesa ya goli la mama, Kwa tukio kubwa kama hili na kashfa nyuma yake naamini wangetoa tamko au neo lolote Kwa wana football

Mashabiki na Watanzania hizi timu zinatupotezea concentration lakini hazipo serious kama tunavodhani, tupambane mambo ya muhimu katika Taifa
Hyjataja mmoja wao SERIKALI.
 
Usiseme "hazipo serious kama tunavyodhani" , sema "hazipo serious kama nilivyodhani" maana tulikuambia muda mrefu toka juzi hiyo mechi itachezwa na hakuna wakupewa points za mezani wewe ukakaza fuvu na maneno kibao ya kujiapiza kuwa labda sio kwa Young Africans.
Na kwa taarifa yako ni wewe tu ndio ulikuwa serious na maneno ya kina Arafat mashabiki wenzako wengi jana baada ya kuliona gari bunju wamefurahia na kushare hiyo habari kwa furaha mitandaoni ikionyesha ni wazi suala la mechi kurudiwa hata wao wanalitamani litokee
 
Atawaalika viongozi wa yanga na Simba ikulu kula nao, atatoa 200 million kwa kila mmoja kwa kigezo cha kulieshimisha taifa kimataifa then atawatangazia kuwa mgeni rasmi kweye derby
Mganga wangu kaniambia hivyo
Tena ukizingatia mwezi wa Ramadhani huu atatoa mwaliko wa Iftaar na picha litaishia hapo
 
Back
Top Bottom