TFF endeleeni kuweka sheria ngumu na adhabu kali kwa mashabiki wanaoleta vurugu viwanjani

TFF endeleeni kuweka sheria ngumu na adhabu kali kwa mashabiki wanaoleta vurugu viwanjani

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2017
Posts
44,855
Reaction score
189,385
Habari,

TFF msicheze wala kuleta utani juu ya mashabiki wanaoleta vurugu viwanjani kwa namna yeyote ile pale inapothibitika tukio kufanyika.

Nimeshangazwa sana na mashabiki wa Simba SC leo kuanza kupiga mashabiki waliokuwa hawa-support timu yao Simba SC.

Ili tukio limewahi kutokea kwa klabu zote kubwa nchini kupiga mashabiki wapinzani na mlitoa onyo na adhabu japo si kali kama mna mpango wa kukomesha hizi tabia.

Pia katika mashindano ya mpira mashabiki wamekuwa na kasumba ya kurusha chupa za maji na takataka viwanjani kupiga wachezaji wakati wanashangilia.

Haya yote TFF mkiwa na huruma mtalea tabia chafu na huko mbele itakuwa ngumu kukomesha kama msipoanza mapema kwa kuchukua adhabu kali bila kujali ni timu gani imeleta vurugu.

Ni heri kukosa mapato kwa baadhi ya mechi Ila adhabu ichukue mkondo wake la sivyo huko baadae tutajilaumu na tutakuwa tumechelewa.

Angalia ligi zilizoendelea ambako siku zote tunatamani kufika huko hakuna mambo hayo zaidi ya kupambana na ubaguzi wa rangi.

Pamoja na yote kwenye ubaguzi wa rangi sheria zilikuwa kali hata kufungiwa mashabiki kabisa sasa sisi huku bongo tunajipagua kwa kupigana wenyewe kwa wenyewe.

TFF msiogope wala msiwe wanyonge sheria zinavyokuwa kali amini amini nawaambiwa huu ujinga utakoma mara moja.

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu.
 
Siungi mkono vurugu hasa za kupigana kwa mashabiki wa soka hususan wa Simba na Yanga.

Lakini nimeona maranyingi mechi za Simba za kimataifa mashabiki wa Yanga wanakuepo na hawapigwi,labda ilo tukio la leo kuna shabiki wa Yanga aliwachokoza mashabiki wa Simba utani wa kuvuka mipaka kama matusi au vinginevyo.
 
Mimi nilikuwepo eneo la tukio, kuna shabiki mmoja wa Yanga alimtukania jamaa mamake, level ya uvumilivu ilikuwa ni ndogo kwa aliyetukaniwa mama ndo ugomvi ulipoanzia.

Ile jamaa wa yanga kutaka kupiganaashabiki wa simba wakaamka kwa hasira na kumshushia kipigo kikali.

Hata humu Jf kuna watu wana utani uliovuka mipaka, laiti kama isimgekuwa anonymity wengi wangekuwa wamechezea vichapo.
 
JESHI LA POLICE MSIPOCHUKUA HATUA KWA HAWA WACHOCHEZI...

Screenshot_2022-02-13-22-47-57-634_com.android.chrome.jpg
 
Sisi tunawakilisha nchi wao wanaleta ujinga, ni haki yao kufukuzwa. Ingelikua Simba na Mtibwa sawa, ila linapokuja suala la kuwakilisha nchi walitakiwa waweke uyanga wao pembeni otherwise wasije uwanjani.
 
Siungi mkono vurugu hasa za kupigana kwa mashabiki wa soka hususan wa Simba na Yanga.

Lakini nimeona maranyingi mechi za Simba za kimataifa mashabiki wa Yanga wanakuepo na hawapigwi,labda ilo tukio la leo kuna shabiki wa Yanga aliwachokoza mashabiki wa Simba utani wa kuvuka mipaka kama matusi au vinginevyo.
Mkuu Umeona Vyema Zile Vurugu Maana Ni Mashabiki Wengi Wakimshambulia, TFF Ichukue Njia Sahihi Fatilia Tukio Na Ikithibitika Basi Sheria Zichukue Mkondo Wake Kukomesha Haya.

Huko Mbele Tutakuja Kushindwa Kuthibiti Haya Kama Tusipowahi Kuchukua Hatua.
 
Mimi nilikuwepo eneo la tukio, kuna shabiki mmoja wa Yanga alimtukania jamaa mamake, level ya uvumilivu ilikuwa ni ndogo kwa aliyetukaniwa mama ndo ugomvi ulipoanzia.

Ile jamaa wa yanga kutaka kupiganaashabiki wa simba wakaamka kwa hasira na kumshushia kipigo kikali.

Hata humu Jf kuna watu wana utani uliovuka mipaka, laiti kama isimgekuwa anonymity wengi wangekuwa wamechezea vichapo.
Kuna Njia Sahihi Za Kushughulika Na Matukio Hayo Maana Kuamka Na Kuanza Kumshushia Kipigo Kizito Kuna Chafua Soka Letu Na Klabu Husika.
 
Back
Top Bottom