Scars
JF-Expert Member
- Apr 8, 2017
- 48,055
- 116,512
Sihalalishi na wala sifurahishwi na tuko hilo, ila najaribu kulielezea katika angle ambayo wewe hukujaribu kuiongeleaKwahiyo Mkuu Unataka Kuhalalisha Njia Iliyotumika Ya Mashabiki Zaidi Ya Ishirini Kumshambulia Shabiki Mpinzani?
Umeongelea upande mmoja wa mashabiki wa Simba as if ndiko tatizo lilipoanzia jambo ambalo linaleta tafsiri ya kwamba mashabiki wa Simba hawapendi kuona mashabiki wa Yanga wakiingia kushanglia timu pinzani na simba na ndio maana wanawaletea fujo mashabiki wa Yanga
Kitu ambacho binafsi nimeona hakipo sawa, kwasababu tunazo record za mashabiki wa Yanga kuingia uwanjani kwenye mechi anazocheza Simba na hatujawahi kusikia mashabiki hao wamepigwa na tena unakuta hata katika zile mechi ambazo Simba anafungwa ambazo ni rahisi sana kwa mashabiki kuwa na hasira na kufanya mazingira ya ugomvi yawe rahisi lakini bado hatukuwahi kusikia kuna Shabiki wa Yanga amepigwa
Zipo clip zinazoenea zikionesha mashabiki wa yanga walivyokuwa huru kutoa maoni yao kwa waaandishi wa habari baada ya mpira kumalizia ambapo walikuwa wamezungukwa na lundo la mashabiki wa Simba huku wakimfuta jasho kila baada ya sekunde kadhaa pindi anapotoa maoni yake, hiyo ni love inayo thibitisha kwamba we treat you as a neighbor not an enemy