TFF endeleeni kuweka sheria ngumu na adhabu kali kwa mashabiki wanaoleta vurugu viwanjani

Kwahiyo Mkuu Unataka Kuhalalisha Njia Iliyotumika Ya Mashabiki Zaidi Ya Ishirini Kumshambulia Shabiki Mpinzani?
Sihalalishi na wala sifurahishwi na tuko hilo, ila najaribu kulielezea katika angle ambayo wewe hukujaribu kuiongelea

Umeongelea upande mmoja wa mashabiki wa Simba as if ndiko tatizo lilipoanzia jambo ambalo linaleta tafsiri ya kwamba mashabiki wa Simba hawapendi kuona mashabiki wa Yanga wakiingia kushanglia timu pinzani na simba na ndio maana wanawaletea fujo mashabiki wa Yanga

Kitu ambacho binafsi nimeona hakipo sawa, kwasababu tunazo record za mashabiki wa Yanga kuingia uwanjani kwenye mechi anazocheza Simba na hatujawahi kusikia mashabiki hao wamepigwa na tena unakuta hata katika zile mechi ambazo Simba anafungwa ambazo ni rahisi sana kwa mashabiki kuwa na hasira na kufanya mazingira ya ugomvi yawe rahisi lakini bado hatukuwahi kusikia kuna Shabiki wa Yanga amepigwa

Zipo clip zinazoenea zikionesha mashabiki wa yanga walivyokuwa huru kutoa maoni yao kwa waaandishi wa habari baada ya mpira kumalizia ambapo walikuwa wamezungukwa na lundo la mashabiki wa Simba huku wakimfuta jasho kila baada ya sekunde kadhaa pindi anapotoa maoni yake, hiyo ni love inayo thibitisha kwamba we treat you as a neighbor not an enemy
 
Hamna kazi za kufanya au?kaeni nyumbani muangalie via Tv mkija uwanjani tutawatwagà tu
Sasa wewe umtwangwe nani? Mtu ambae naweza hata kukununua, hizi fake ID (anonymity) zinawapa kiburi sana mafukara wa Jf.
 
Waambie waweke stewards majukwaani,siyo kukusanya tu mapato ya uwanja
 
Hali Mbaya Sana Kuna Kazi Kubwa Kwa Wadau Na Wapenda Mpira Kupewa Elimu Elekezi Maana Hata Hizi Comments Chache Zinadhihirisha.
Utakuwa mpuuzi na level ya ustaarabu kwako ni km shimo la choo!!.
 
Hujanielewa mkuu, kuna kipindi inafika uvumilivu unaisha kabisa yani. Mtu unamzuia ila anaendelea.
Pia Tukio Hilo Liliambatana Kwa Kupiga Mashabiki Wote Pinzani Pitia Video Za Marejeo Utashuhudia Tukio Nzima La Hovyo.
 
Mkuu Tukio Hili Umeona Ambavyo Limetokea Si Shabiki Mmoja Kupigwa Pekee Bali Mashabiki Pinzani Kulazimishwa Kutoka Nje Ya Uwanja Kwa Nguvu Na Kurushiwa Chupa Pia.


Na Kumbuka Sheria Uchukua Nafasi Pale Kosa Linapotendeka Haijalishi Nyuma Ulifanya Nini.

Nawakumbusha TFF Wachukue Hatua Ili Kukomesha Hizi Vurugu.

Pia Kuweka Walinzi Majukwaani Kusaidia Kuongeza Hali Ya Usalama Viwanjani.
 
Yalipotokea huko nyuma kwa team ya Simba sc ulileta uzi hapa kushinikiza Yanga waadhibiwe?
 
Wakati ule mashabiki wa Simba Sc wamepigwa kule morogoro kwenye mechi ya Yanga ulileta uzi?
Sikupata Kushuhudia Yaliyokea Ila Hili Nimeshuhudia Na Kuona.

Pia Inawezekana Ushiriki Wangu Hapa JF Ulikuwa Ni Mdogo.
 
Ungewasisitiza kuweka ulinzi majukwaani na siyo kukusanya tu mapato ya mlangoni.usalama wa hao waloingia uwanjani ni muhimu zaidi.
 
Husuda na chuki tu ?!

Yani swala la Shafii linasikitisha wengi sana!

Kwamba mahususi kosa lake ni gani ?

Kwa adhabu kubwa kiasi kile ?!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…