TFF HAMUWEZI KUENDESHA MPIRA ,

TFF HAMUWEZI KUENDESHA MPIRA ,

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2014
Posts
24,501
Reaction score
28,711
Ili ligi ikue zaidi, inatakiwa pia kombe(trophy) liwe kama identity pia, Yanga alipochukua ubingwa mara 3 alipewa makombe yenye muonekano tofauti, nilijiuliza hivi kweli hii ni ligi au bonanza ,? Nikajiuliza hivi kwanini mpira wetu unaendeshwa na mambumbu?

Pale uingereza wana aina moja ya taji la ligi kuu toka 1992, halibadiliki badiliki ovyo, na haitakiwi mtu alikopi , hiyo pia inaongeza brand ya ligi, hebu fikiria kila msimu pale EPL, au laliga wangekuwa wanakurupuka na miundo tofauti ya mataji ya ligi kuu,

Tff inaendeshwa na wachumia tumbo,wasiojifunza kinachoendelea duniani, ndio maana timu moja inakuwa na viporo 10, kipind kama hiki inajulikana ratiba ya CAF, na michuano mingine , lakin msimu ujao ratiba itachezewa ovyo ovyo ,

Natamani siku moja mpira wa Tanzania wapewe wanaoujua mpira na kuufikisha sehemu Fulani,

Kwa ligi yetu kwasasa bingwa alitakiwa awe anapata angalau million 300, lakin eti anapewa million 80, na mwaka huu haijulikani, huenda asipate chochote,

ANGALIA. ..HAYA MAKOMBE YOTE ETI YA LIGI KUU TANZANIA LAKINI kila akija kiongoz anakuja na muundo wake , hii haikubaliki , soka letu mnalizika taratibu
tapatalk_1559069367255.jpeg
Pg-32.jpeg
Yanga-2-.jpeg
 
Yanga inawauma sana mezeni panadol, mtazoea tu. Na mdogo wenu dadeki kashuka akatusubirie huko. Tutakutana federation cup
 
Umeandika point mkuu!! Tz hatuna proffessional leaders/experts wa michezo na miundo mbinu yt ya michezo bali yyt yule anapewa kitengo na uzoefu na Akili ya uongozi atapatia katikati ya majukum ya hicho kitengo hivyo inadhoofisha uendeshaji. Wanaopewa majukumu ni rushwa tu kujichumia hela fasta na hawawazi kuendeleza sekta ya michezo.

Kwa upande wa kombe na gawio au thamani yake, tubajeti chetu tudogo hlf hatuna serous investment kweny hii sekta...it is not the priority in such!! Bingwa ajulikane, tupite hiv
 
Ligi imeisha kwa mafanikio makubwa,huko CAF tumefanikiwa kuingiza timu 4 baada ya Simba kutinga robo ya mashindano CCL jambo ambalo awamu za nyuma hawakuwahi kulifikia.We una lako jambo...!
 
Basi mwakani mchukue nyie Yanga fc, hilo Kombe ili hao TFF waweze kuendeleza mpira.
Mna kelele sana kwa Simba kuchukua hili Kombe la TPL hadi mna kera.
Chukueni ubingwa wa TPL msimu ujao.
Ili hilo Kombe liwe na thamani.
 
Yanga inawauma sana mezeni panadol, mtazoea tu. Na mdogo wenu dadeki kashuka akatusubirie huko. Tutakutana federation cup
We Mbumbumbu wenzio wanajadili vitu vya msingi we unaingizia ukiazi wako hapa.
 
Nye vyura ukitokea mwakani mkachukua ubingwa hilo kombe hamwezi kulichukua?
 
Katika awamu hii tff imevuka malengo team ya simba imeweza kufika robo fainali club bingwa pia team ya taifa imefudhu Africon, Big Up tff kazi nzuri viongozi waliopita tff hawakuweza kufikia mafanikio haya KARIA Big Up Sana tunahitaji uwakilishi wa simba uendelee mwakani tutafika nusu fainali ikiwezekana tubebe ndoo kabisa, pia Team ya Taifa tutaenda World Cup
 
Asante kwa kudadavua kwa ufasaha mafanikio ya TFF katika msimu huu wa Ligi ya TPL chini ya Rais wake Karia.
Yanga fc wanayatazama mafanikio ya Ligi ikiwa tu wao watakuwa mabingwa wa TPL.
Big up TFF
 
Ili ligi ikue zaidi, inatakiwa pia kombe(trophy) liwe kama identity pia, Yanga alipochukua ubingwa mara 3 alipewa makombe yenye muonekano tofauti, nilijiuliza hivi kweli hii ni ligi au bonanza ,? Nikajiuliza hivi kwanini mpira wetu unaendeshwa na mambumbu?

Pale uingereza wana aina moja ya taji la ligi kuu toka 1992, halibadiliki badiliki ovyo, na haitakiwi mtu alikopi , hiyo pia inaongeza brand ya ligi, hebu fikiria kila msimu pale EPL, au laliga wangekuwa wanakurupuka na miundo tofauti ya mataji ya ligi kuu,

Tff inaendeshwa na wachumia tumbo,wasiojifunza kinachoendelea duniani, ndio maana timu moja inakuwa na viporo 10, kipind kama hiki inajulikana ratiba ya CAF, na michuano mingine , lakin msimu ujao ratiba itachezewa ovyo ovyo ,

Natamani siku moja mpira wa Tanzania wapewe wanaoujua mpira na kuufikisha sehemu Fulani,

Kwa ligi yetu kwasasa bingwa alitakiwa awe anapata angalau million 300, lakin eti anapewa million 80, na mwaka huu haijulikani, huenda asipate chochote,

ANGALIA. ..HAYA MAKOMBE YOTE ETI YA LIGI KUU TANZANIA LAKINI kila akija kiongoz anakuja na muundo wake , hii haikubaliki , soka letu mnalizika taratibuView attachment 1110820View attachment 1110822View attachment 1110821
Usiseme Tff Sema Viongozi Hawa Wa Tff Hawawezi Kuongoza Mpira
 
Ilo kombe limechongwa kwa mafundi chuma pale Temeke mwisho kwa elfu 50 tu
 
Back
Top Bottom