Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 13,667
- 21,296
Ni wazi Yanga imekiuka kanuni za FIFA kwa kushiriki kampeni za CCM katika uchaguzi mkuu wa kisiasa kupata viongozi wa serikali. Kwa hiyo ili kuepuka rungu la FIFA na kulinda heshima ya nchi kimichezo lazima TFF ichukue hatua za kuiadhibu Yanga ikiwa na pamoja na kuifungia kushiriki mashindano yo yote ya kitaifa na kimataifa.
Inafahamika kuwa viongozi wote wa TFF ni makada wa CCM lakini sheria ni msumeno lazima Yanga ipate adhabu kali bila huruma vinginevyo TFF iadhibiwe kwa kufungiwa katika shughuli zote za mpira wa miguu kimataifa.
Athari za TFF kufungiwa ni kuwa hakuna timu yo yote ya Tanzania itaruhusiwa kushiriki mashindano yo yote ya kimataifa.
Wito kwa TFF ni kuchukua hatua za kuiadhibu Yanga haraka iwezekanavyo!