Viol
JF-Expert Member
- Dec 15, 2009
- 25,420
- 18,298
TFF imemfungia mwamuzi msaidizi mechi ya Simba vs Namungo miaka 3 kutoka na kushindwa kuitafsiri sheria ya offside.
===
TFF WACHOMOA 'BETRI' KWA MWAMUZI ALIYECHEZESHA SIMBA VS NAMUNGO, AFUNGIWA MIAKA 3
NA ANDREW CHALE.
KAMATI ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imemfungia Mwamuzi msaidizi namba mbili Kassim Safisha miaka mitatu (3) kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea katika iliyowakutanisha simba dhidi ya Namungo fc mechi hiyo iliyochezwa Januari 29,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa mchana wa leo na Afisa habari na Mawasiliano wa TFF,
Cliford Mario Ndimbo ilieleza kuwa, Adhabu hiyo imetolewa kwa mujibu wa Kanuni namba 39 (1) (a) ya Ligi Kuu kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
Aidha, katika kikao hicho ilipitia mwenendo mingine na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao.
Ligi Kuu ya Vodacom, mechi namba 157: Azam FC 1 v Mtibwa FC 1-Mwamuzi Meshack Suda ameandikiwa barua ya kukumbushwa kufanya majukumu yake kwa umakini zaidi katika mechi iliyochezwa Januari 30,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Vile vile katika mchezo huo Kamishina Abdallah Zongo ameondolewa kwenye orodha ya Makamishina kwa kosa la kutoa taarifa yenye mapungufu.Adhabu hii ni kwa kuzingatia Kanuni namba 40(1) kuhusu Udhibiti Kamishina
Mwisho.
Sent using Jamii Forums mobile app