VOICE OF MTWARA
JF-Expert Member
- Dec 20, 2012
- 2,987
- 1,954
nimesikitishwa sana na kitendo cha mwamuzi wa mechi hiyo kwa kitendo chake cha kumaliza mpira wakati mshambuliaji wa MGAMBO yuko pekeyake mbele ya kipa wa AZAM na uwezekano wa mshambuliaji yule kufunga ni asilimia 98.
kama kweli TFF wana dhamira ya dhati ya kuendeleza soka la Tanzania basi wamwadhibu mwamuzi huyu.
Viongozi wao hawajataka kupigana leo?
Mpira ni dakika 90 tu. Muda ukiisha kipenga ni lazima kipulizwe. Endapo goli lingefungwa nje ya muda hilo bao lingekuwa disputed kwa kufungwa kinyume na sheria 17 za soka.
Mimi nadhani tusiyumbishwe na hisia zetu za kutaka kuona Azam anafungwa bali tusimame katika haki. Maadam muda uliisha na mfungaji alikuwa hajafunga, kipenga kilimaliza mambo yote.
mkuu umetazama mchezo husika?
Mtujuze matokeo ya mechi hiyo
Mgambo 0-0 Azam
Mtibwa 1-0 Prisons
Simba tushindwe wenyewe...
Hamuwezi, kama Kapeto ni wa kubaki hapahapa, nayo Simba ni ya kubaki nafasi ya 3. Mkijitutumua kumfunga Azam mtaifanya Yanga itangaze ubingwa mapema sana. Kuweni makini mnapofukuzia nafasi ya pili.
unataka kusema nafasi ya tatu kwetu Bado Ni kitenda wili...
teh teh teh Tanzania kuna vituko sana, mmiliki wa azam fc ndio mdhamini wa ligi kuu. Kwa hiyo azam fc inamiliki timu zote za ligi kuu. Wameishindwa Yanga tu.!!
Mkuu sikuangalia nilikuwa shambani. Radio One wamesema goli lilifungwa kabla ya kipenga, ukweli ni upi?