TFF inapata ugumu gani kumtangaza mdhamini kuu Tanzania TPL??

Bujoro

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
3,115
Reaction score
2,231
Habar za leo viongozi wamgu, kabla ya yote naeasalimu wote...

Na baada ya Salaam naomba nijielekeze moja kwa moja hadi kwenye mada husika kama ambavo kicha cha habar kinasomeka jmn watanzania wenzangu hivi mnamfahamu mdhamini wa ligi yetu pendwa kuu ya Tanzania yaani TPL!?? Maana mwka jana ligi imeisha bila ya mdhamini sasa hii sio haki maana vilabu vipata wakat mgumu kuniendesha tunona baadhi ya timu zikipambana sana hata kupata nauli ya kusafuri kwenda kucheza mechi za ligi kuu sasa haya mambo hatutaki yatokeee tena msimu huu wa 2019 na 20

Tff walijinasibu kuwa mpaka ligi inaanza watakuwa wamemtangaza mdhamini na leo ni tar 21 maana yake bado siku 1 ligi kuu kuanza na wajamtangaza, maana yake ni nn au kuna shida au tatizo gani mpaka mdhamini afanywe kuwa siri kubwa na nzito kama vile ni issues za kuuza madawa ya kurevya??

Au labda walishamtangaza mimi tu ndo sina Habari?? Naombeni mnijuze jmn na kama ni bado je tff wanatutendea haki wa Tanzania na mpira wa miguu Nchini!?? Waambieeni waache mazoea now sisi sio wajinga kiasi hicho tumepevuka sasa wawe serous kwenye mambo serious kama haya ya Kitaifa...Tff inabidi wajitafakari sana sio poa hata robo..tunataka mpira wa nchi upige hatua sio kurudi nyumba makitaimu kila mwaka Tpl mi brand kubwa sio ya kukosa mdhamini mpaka sasa.. Naomba kuwasilisha.
 
Kama hayupo unataka watangaze hewa??kama angekuwapo na kila kitu kimekamilika unadhani wangesuburi kutangaza??Note than EPL yenyewe haina mdhamini mwaka wa 4 huu sijui usidhani hawataki
 
Note than EPL yenyewe haina mdhamini mwaka wa 4 huu sijui usidhani hawataki

We Kijana ni mwongo sana
Epl haijawahi kukosa tittle sponsor

Tittle sponsor wa Epl aliyemaliza mkataba wake alikuwa ni Barclays bank
Wataalamu wenye ligi yao wakakataa kuongeza mkataba mwingine Kwasababu walifanya research wakaona tittle sponsor hana faida Kwasababu Epl tayari ni maarufu kuliko Barclays yenyewe

Hivi kama wewe ni mfuatilaji wa soka unaweza kusema Epl inakosa mdhamini ?Kwanini mnapenda kuzusha habari wakati hamjui?

Ligi ya Tanzania imekosa tittle sponsor sio kwamba wadhamini Hakuna
Karibu kila club inawadhamini leo nimeangalia club ya kinondoni fc imesaini mkataba wa bilion tano za udhamini je huoni huo ni udhamini?
 
Udhamini sio lazima wala haki, ila ni busara. Ukishakubali kucheza ligi basi jiandae na gharama zake pia. Tuwapongeze TFF kwa jitihada za kutafuta mdhamini
 
KMC?
 
vilabu vingine havina hao wa dhambi udhani vitajindeshaje aisee

Rekebisha hapo
Naomba nikufahamishe sio jukumu la Tff kutafutia vilabu udhamini hiyo Sio Tanzania tu Ni duniani kote

Kazi ya Tff ni kusimamia na kuongoza na kutoa zawadi kwa washindi sema ligi hii bado haiendeshwi kitaalamu ndio unakuta club hata haziwezi kulipa mshahara Wachezaji
Tuseme ligi yetu bado sio professional

Club ambayo haiwezi kutafuta mdhamini wake hata akija tittle sponsor sioni ikipata nafuu
Kumbuka kazi ya tittle sponsor kwa Tanzania hutoa kits kwa ajili ya maandalizi ya ligi pamoja na facilities zingine ndogo ndogo

Na sio kwamba ligi yetu haina wadhamini wapo Azam t.v. wapo KBC

Nilitoa mfano hapo juu wa ligi ya Uingereza Epl yenyewe hategemei tittle sponsor ili kundesha ligi kutokana na anaingiza mapato makubwa sana kwa msimu A billion dollars

Pamoja na kuwa tff inamapungufu ila vilabu vyetu pia vimelala bado hawapo serious na biashara ya mpira

Je laliga kuna tittle sponsor? Bundesliga je ? Series A?

Inahitaji transformation kubwa Kwenye mpira wa kitanzania kwa sababu mashabiki wapo
Mpira utoke Kwenye usela na Ujanja ujanja
 
Ni Bilioni 1. Kila mwaka 200ML kwa miaka mi 5
 

Nakubaliana na wewe kwenye hoja zako kadhaa hapo juu kama ulivyozieleza vema.
Lakini bado hoja ya mleta uzi ina mashiko, bado ligi yetu inahitaji mdhamini mkuu (league's main/title sponsor).
Ikumbukwe hata EPL ni baada ya kukua na kujitosheleza ndio wakaachana na mdhamini (wa ligi) Barclays Bank.

Kama sote tunakubaliana kwamba kwa hatua tuliyopo kimpira bado tunamhitaji mdhamini mkuu wa ligi, basi kuna maswali kadhaa ni lazima tujiulize....

1. Kwanini hadi sasa mdhamini mkuu hajatangazwa ?
2. Je, TFF na bodi ya ligi wameshindwa kumpata mdhamini mkuu ?

3. Kama wameshindwa (au wameshindwana), wanashindwaje kupata mdhamini muda wote huo tangu ligi ya msimu uliopita imeisha hadi ya msimu huu inataka kuanza ? (Tatizo ni nini ?)

4. Kama ligi itaanza bila ya mdhamini mkuu, je, ni sahihi kwa ukubwa wa ligi yetu kuchezwa huku ikiwa haijulikani mshindi (timu bingwa wa ligi) na washindi mbalimbali (wachezaji, makocha na waamuzi, timu yenye nidhamu, n.k) watapata zawadi gani (kama msimu uliopita) ?

5. Je, ni sawa kuendelea kuwapo ofisini kwa viongozi wa shirikisho walioshindwa kusimamia jambo la msingi na zito kama hili ?

NB; Naamini mleta uzi amehoji kwa wema kabisa akiamini kwamba mambo haya yalistahili kuwa bora zaidi ya yalivyo sasa. Namimi nina muunga mkono kwa hilo kama ambavyo mpenda michezo yoyote yule angefanya.
 
Labda ni Rostam Aziz, sasa kama yeye Karia anashirikiana na serikali kuwafunga wadau wenzake wa michezo kisa ni wapinzani wake, unafikiri ni nani atakuwa tayari kushurikiana naye.
 
Nitangulize ku
Hiv mkuu, zile Santander na La BBVA si ni wadhamin wa la liga kwa vipindi tofaut tofaut au vp!!?
 
Kama hayupo unataka watangaze hewa??kama angekuwapo na kila kitu kimekamilika unadhani wangesuburi kutangaza??Note than EPL yenyewe haina mdhamini mwaka wa 4 huu sijui usidhani hawataki
.

EPL naona ina wadhamini kila nyanja mfano.


Time keeper- TAG Heuer
Ball- Nike
Drinks- Coca-Cola
Snacks- nimesahau.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…