Naunga mkono hoja kwa maana ya marekebisho ktk msimu ujao. Haipendezi timu kupewa ushindi wa mezani.
Ni kweli pia kuwa kama Simba angeshinda hii mechi huku Kagera akiwa na mchezaji mwenye kadi 3 inaonekana asingeonekana na hivyo kosa lisingeadhibiwa. Kanuni irekebishwe ili unapochezesha mchezaji mwenye kadi 3 unyang'anywe tu point hizo hizo tatu hata kama hapewi mtu yeyote, otherwise hakuna faida ya kuwa na adhabu ya kadi!
Lakini hiyo ni marekebisho yajayo kwa sasa hivi hakuna namna, ni TFF kuamua kwa mujibu wa kanuni iliopo na ushahidi uliopo mbele yao.
Huku kuzungazunguka ni kutaka kuficha au kuharibu ushahidi uliopo ambao unaonyesha Fakhi ana kadi 3!
Kwenye issue ya Haji Manara, alichofanya hakina tofauti na alichofanya Salum Mkemi kutoa povu kabla ya uamuzi wa Kamati ya Masaa 72, nimeshangaa sana unashindwaje kuiomba TFF iwaadhibu wote.