Sio kazi ya kocha wa taifa kukuza uwezo wa wachezaji wetu. Kosa lake ni kuchagua wachezaji kutokana na timu na maeneo wanayotoka na si kwa uwez wao.
mf, viungo wote walioitwa ni wagumu hakuna mbunifu pale hata mmoja lakini Awesu Awesu ameachwa sababu tu anatokea KMC Fc.
Pia mchezaji kama Kibu anakosaje nafasi ya kucheza kwenye hii timu?
SIjaona sababu ya msingi ya kuwaacha Kijili, Mzize na Ally Salim. Kwa sasa Ally Salim ni kipa bora kuliko wote wale walioitwa.
Ao walioteuliwa ndio afadhali kidogo lakini kwa Level inayochezwa AFCON ni sahihi alivyo sema kocha tunakwenda kujifunza.
Hatuna wachezaji hata mmoja wa kushindana tuna wachezaji wa kushiriki.
Ni kama tunavyo wacheka Zalani ya South Sudan wakijabkushiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika apa DSM dhidi ya timu zetu Pendwa.
Kinachohitajika ni kuandaa miundombinu na walimu kuanzia grassroot uko.
Uwe mkakati maaluma ambao Serikali inahitajika iweke fedha ya kutosha (billions) na wasimamizi makini na uwe mpango endelevu.
Tuki Fanya hivyo tutapata matunda miaka 8/10 ijayo.
Kwasasa Mashindano ya AFCON ni kujidanganya kwenda na level ya Mwamyeto, Kibu n.k kwenda kushindana sio kweli.
Angalia Senegal anavyo mtesa Cameroon,vijana wadogo 20/26 wamoto, wanakimbiza hatari.
Cheki Morocco, vijana wadogo 20/26 wanakimbiza muda wote.
Kama hatutaki kuweka fedha basi tusi lalamike.
Tunashiriki kwa mara ya tatu hatujawahi kupata point 3.