Lupweko
JF-Expert Member
- Mar 26, 2009
- 23,566
- 24,891
Wapenzi wa soka walioshuhudia pambano la watani wa jadi hapo jana watakuwa ni mashahidi wa kiwango duni kabisa cha uchezeshaji kutoka kwa mwamuzi Martin Saanya. Hakuna haja ya kurudia rudia kutaja makosa yake yasiyo ya kibinadamu, bali ya makusudi, ila ili hoja isimame kutaja baadhi tu ni lile la kukataa bao halali la Ibrahimu Ajibu wa Simba, kuruhusu bao lisilo halali la Amis Tambwe wa Yanga na kumtoa nje kwa kadi nyekundu nahodha wa Simba ambaye kimsingi ndiye walau kwa cheo chake cha unahodha alikuwa anaruhusiwa kuhoji uamuzi mbovu uliokuwa unaendelea.
Ni jambo la dhahiri kuwa huyu mwamuzi atafungiwa na TFF kuchezesha mpira wa soka, hilo halina ubishi na litatokea tu. Rai yangu ni kwamba mbali na adhabu hiyo, mwamuzi huyo pia asilipwe posho ya kuchezesha pambano la jana, na pia kama bado atakuwa ana roho ngumu ya kuendelea na kazi ya uamuzi, basi hata atakapomaliza adhabu alipe faini ili fedha hizo za posho yake na faini zitumike kukarabati walau viti kumi kati ya zaidi ya viti mia mbili vilivyoharibiwa na mashabiki wenye hasira
Hii itawafanya waamuzi waheshimu taaluma hiyo, maana huyu jamaa ana historia ya kuvurunda na kufungiwa kuchezesha, lakini hajifunzi. Hata jana alikuwa anachezesha pambano hilo kwa kuwa alikuwa amenufaika na 'msamaha wa rais wa TFF' alipoingia madarakani na kuwaachia huru waamuzi waliofungiwa, sasa ajabu ni kwamba ameshindwa hata kuthamini msamaha aliopewa, na heshima pia aliyopewa kuchezesha pambano kubwa kama la jana.
Napendekeza asilipwe posho wala nauli ya kurudi Arusha, na akitaka kurudi baada ya kumaliza kifungo (maana najua lazima atafungiwa walau mwaka mmoja), alipishwe faini ya kutikisa mfuko wake