TFF isimlipe posho mwamuzi Martin Saanya

Lupweko

JF-Expert Member
Joined
Mar 26, 2009
Posts
23,566
Reaction score
24,891
Wapenzi wa soka walioshuhudia pambano la watani wa jadi hapo jana watakuwa ni mashahidi wa kiwango duni kabisa cha uchezeshaji kutoka kwa mwamuzi Martin Saanya. Hakuna haja ya kurudia rudia kutaja makosa yake yasiyo ya kibinadamu, bali ya makusudi, ila ili hoja isimame kutaja baadhi tu ni lile la kukataa bao halali la Ibrahimu Ajibu wa Simba, kuruhusu bao lisilo halali la Amis Tambwe wa Yanga na kumtoa nje kwa kadi nyekundu nahodha wa Simba ambaye kimsingi ndiye walau kwa cheo chake cha unahodha alikuwa anaruhusiwa kuhoji uamuzi mbovu uliokuwa unaendelea.

Ni jambo la dhahiri kuwa huyu mwamuzi atafungiwa na TFF kuchezesha mpira wa soka, hilo halina ubishi na litatokea tu. Rai yangu ni kwamba mbali na adhabu hiyo, mwamuzi huyo pia asilipwe posho ya kuchezesha pambano la jana, na pia kama bado atakuwa ana roho ngumu ya kuendelea na kazi ya uamuzi, basi hata atakapomaliza adhabu alipe faini ili fedha hizo za posho yake na faini zitumike kukarabati walau viti kumi kati ya zaidi ya viti mia mbili vilivyoharibiwa na mashabiki wenye hasira

Hii itawafanya waamuzi waheshimu taaluma hiyo, maana huyu jamaa ana historia ya kuvurunda na kufungiwa kuchezesha, lakini hajifunzi. Hata jana alikuwa anachezesha pambano hilo kwa kuwa alikuwa amenufaika na 'msamaha wa rais wa TFF' alipoingia madarakani na kuwaachia huru waamuzi waliofungiwa, sasa ajabu ni kwamba ameshindwa hata kuthamini msamaha aliopewa, na heshima pia aliyopewa kuchezesha pambano kubwa kama la jana.

Napendekeza asilipwe posho wala nauli ya kurudi Arusha, na akitaka kurudi baada ya kumaliza kifungo (maana najua lazima atafungiwa walau mwaka mmoja), alipishwe faini ya kutikisa mfuko wake
 
Maamuzi sahihi maamuzi ya haki maamuzi ya kufuata sheria taratibu na kanuni kwenye chochote ni jambo muhimu sana.. jana yangetokea maafa achilia mbali uharibifu uliofanyika huyu saa hii angekuwa lockup
Na TFF walifanya kosa kubwa kumpa kazi ya kuchezesha mechi kama ile mtu aliyetoka kifungoni na mwenye historia ya kuharibu
Hata mashabiki wa Yanga jana hawa kushangilia kwa furaha waliona aibu kwa kuzawadiwa bao la mkono
Inawezekana kabisa rangi huathiri hata maamuzi yetu! Nikiangalia rangi za ccm na yanga......![emoji144] [emoji144] [emoji144]
 
Et refa alikua anamuogopa boss wake aliekua jukwaan....
 
Wapenzi wa soka walioshuhudia pambano la watani wa jadi hapo jana watakuwa ni mashahidi wa kiwango duni kabisa cha uchezeshaji kutoka kwa mwamuzi Martin Saanya. Hakuna haja ya kurudia rudia kutaja makosa yake yasiyo ya kibinadamu, bali ya makusudi, ila ili hoja isimame kutaja baadhi tu ni lile la kukataa bao halali la Ibrahimu Ajibu wa Simba, kuruhusu bao lisilo halali la Amis Tambwe wa Yanga na kumtoa nje kwa kadi nyekundu nahodha wa Simba ambaye kimsingi ndiye walau kwa cheo chake cha unahodha alikuwa anaruhusiwa kuhoji uamuzi mbovu uliokuwa unaendelea.

Ni jambo la dhahiri kuwa huyu mwamuzi atafungiwa na TFF kuchezesha mpira wa soka, hilo halina ubishi na litatokea tu. Rai yangu ni kwamba mbali na adhabu hiyo, mwamuzi huyo pia asilipwe posho ya kuchezesha pambano la jana, na pia kama bado atakuwa ana roho ngumu ya kuendelea na kazi ya uamuzi, basi hata atakapomaliza adhabu alipe faini ili fedha hizo za posho yake na faini zitumike kukarabati walau viti kumi kati ya zaidi ya viti mia mbili vilivyoharibiwa na mashabiki wenye hasira

Hii itawafanya waamuzi waheshimu taaluma hiyo, maana huyu jamaa ana historia ya kuvurunda na kufungiwa kuchezesha, lakini hajifunzi. Hata jana alikuwa anachezesha pambano hilo kwa kuwa alikuwa amenufaika na 'msamaha wa rais wa TFF' alipoingia madarakani na kuwaachia huru waamuzi waliofungiwa, sasa ajabu ni kwamba ameshindwa hata kuthamini msamaha aliopewa, na heshima pia aliyopewa kuchezesha pambano kubwa kama la jana.

Napendekeza asilipwe posho wala nauli ya kurudi Arusha, na akitaka kurudi baada ya kumaliza kifungo (maana najua lazima atafungiwa walau mwaka mmoja), alipishwe faini ya kutikisa mfuko wake
Hivi mnaijua TFF ya Malinzi au mnaisikia mnaweza sikia huyo refa anapongezwa na kupewa tuzo.
 
Tatizo Simba kwa ujumla wake waliingia na matokeo yao uwanjani kabla ya mchezo ili wafute unyonge wao kwa Yanga na mchezo ukawa tofauti na matokeo waliyonayo. Hongereni Simba kwa ushindi.
 
kesha lipwa huyo, kuna mdau mmoja aliwah kunambia kuwa tangu rais mpya wa TFF aingie madarakan ikitokea game ya watani simba na yanga harafu yanga akashinda, refarii aliyechezesha game hiyo hulipwa fasta sana tena na nyongeza juu, ila kinyume chake yaan ashinde simba inasemekana refarii atasota sana ofic za tff akidai chake but huambulia kapa.
 
asifungiwe tu kuchezesha bali afungwe jela ya kawaida walau miezi mitatu
 
Back
Top Bottom