Naunga mkono hoja yako na duniani kote ndivyo ilivyo. Lakini ni nyie hao hao mliokuwa mnamhasisha Nyoso awavunje miguu Wachezaji Fulani. Ushabiki maandazi ukipokelewa na Wachezaji bichwa nazi matokeo yake ndo haya ya Mchezaji mzuri kama Phiri kukaa nje ya uwanja zaidi ya mwezi huku timu yake ikiwa na mashindano Makubwa.Ligi yetu imekuwa sana, inavutia wachezaji wakubwa wa kimatifa kuja kucheza hapa. Wachezaji hawa wanaokuja kwetu wanategewa sana sio TU na club zilizowanunua bali hata na timu zao za mataifa wanatoka, sio jambo zuri hata kidogo kama wachezaji hawa wataumizwa kwa makusudi TU na wavuta bangi,
TFF kuweni wakali sana kwa wachezaji wanaocheza faulu za makusudi kuumiza wachezaji wengine na marefa ambao hawachukui hatua kwa wachezaji wakorofi kwakuwa ligi yetu Inafuatiliwa sana Kimataifa.
Sio jambo zuri na ni aibu kuona Tanzania hakuna mwamuzi hata mmoja aliyeshiriki kombe la dunia.
Kulinda wachezaji ni kuwa na marefa wenye weledi wanaofuata sheria 17 na kanuni za mchezo ambao wameongezewa VAR kuimarisha maamuzi Yao viwanjani.Kwahiyo wawalinde kwa namna gani? Hebu tupe mbinu wafanyaje ili hao wachezaji walindwe
Sawa mkuu lakini kwa swala la VAR FIFA ndo wanaokupa ruhusa ya kuitumia kwenye ligi yako endapo watakukagua na kukuta umetimiza vigezo.Kulinda wachezaji ni kuwa na marefa wenye weledi wanaofuata sheria 17 na kanuni za mchezo ambao wameongezewa VAR kuimarisha maamuzi Yao viwanjani.
Yaani TFF italinda wachezaji kwa kufanya yafuatayo:
1. Viwanja vyote viwe na dimba zuri
2. Ratiba za mechi himilivu kwa wachezaji
3. Kuwepo kwa ambulance uwanjani full time.
4. Matumizi wa waamuzi vwanaofuata sheria 17 kama zilivyo. Watoe adhabu kama inavyostahili kwa wachezaji wote na timu zote.
5. Kusimamia haki/mikataba ya wachezaji kama inafuata viwango vya FIFA na kushauri kabla mgogoro haujatokea
6. Kutumia VAR, wafuatilie ahadi ya Dr. Mwiguli, waziri wa fedha kuhusu VAR
Ni aibu kwa TFF ligi yetu kushindwa kutoa waamuzi kwenye mashindano makubwa ya Kimataifa.
watoe adhabu stahiki kwa refa by l
TFF ndiyo wenye mpira wao. Swala la kutimiza vigezo vya kutumia VAR ni lao. TFF kwa kutumia busara zao na hekima ya Rais Samia wanaweza kukaa chini na CCM kufanya mazungumzo ya kurejesha baadhi ya viwanja vya mpira kwa TFF ili vipate matunzo na ukarabati kwa viwango vya FIFA. Hili ni lao TFF kukaa na uongozi wa chama kwa mazungumzo yenye maslahi kwa mpira wetu.Sawa mkuu lakini kwa swala la VAR FIFA ndo wanaokupa ruhusa ya kuitumia kwenye ligi yako endapo watakukagua na kukuta umetimiza vigezo.