TFF mara hii mmeshaichoka Simba?Lawama mnayoikwepa inaweza kuwa kubwa zaidi

TFF mara hii mmeshaichoka Simba?Lawama mnayoikwepa inaweza kuwa kubwa zaidi

Mohamed Mbelwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 13, 2013
Posts
507
Reaction score
272
Na. Chiki Mchoma.
+255 712 885 999

Ni kama utata wa dereva wa boda boda au tax.

Pale ambapo ulimwambia utashukia sehemu fulani halafu mkifika sehemu hiyo anakwambia huko mbele siendi shukia hapa tulipokubaliana.

Mwingine hata umwambie nitakuongeza pesa basi yeye atajenga dhana kuwa una nia Ovu na wala siyo ile uliyoonesha awali.Huwezi kuzuia fikra za Mtu.

Yawezekana Simba haikuwa na makubaliano kama ya dereva tax au wa boda boda na TFF lakini ni dhahiri TFF inataka kuonesha kuwa imefikia tamati ya kushirkiana na Simba katika jambo hili la Kitaifa ambalo katika Wafaidika wakuu na TFF wamo.

Najenga dhana kuwa inawezekana kuwa kosa la Simba ni kule kusema tamaa yao ilikuwa ni kufika Robo Fainali na ambayo tayari wameshafika na sasa wameshamalizana na TFF ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakiisaidia Simba kwa misingi ile ile ya Utaifa kwanza.

Simba imekuwa kwenye Mashindano ya Klabu Bingwa Afrika na imekuwa inavuka hatua kwa hatua na TFF ilikuwa na Msaada sahihi na wa nia njema ambao si wao tu ila Nchi zote zenye timu zilizo Klabu Bingwa Afrika kupitia vyama vyao vya Soka vimekuwa vikisaidia Timu zao zilizo kwenye hatua hiyo.

TFF inataka kukwepa hoja ya Viporo vya Simba kwa kuilazimisha Simba kucheza kesho dhidi ya JKT.

Unajiuliza iwapo Simba itacheza kesho dhidi ya JKT kisha keshokutwa mchana ikasafiri kwa Masaa matano mpaka Dar es Salaam ikapumzika kisha Ijumaa ikafanya Mazoezi ambayo kimantiki hayatakuwa na tija yoyote kwa mechi ya Jumamosi dhidi ya TP Mazembe sijui hili ni kwa manufaa ya nani.

TFF kupitia Bodi ya ligi wangeweza kugonga hodi kwa Mkurugenzi wa Michezo Bw. Ammy Ninje na kumuuliza juu japo uungwana wa hilo.

Hili la iwapo Simba ikaibua majeruhi (hatuombei na hata TFF haiombei) au ikapata uchovu (fatique) utakaoipa timu ubora dhaifu wa mchezo wao dhidi ya Mazembe ninyi mtakuwa na nafasi kubwa ya kulaumiwa.

Zipo faida nyingi ambazo TFF inazijua kuwa zitakuwa zake moja kwa moja iwapo Simba itapewa nafasi ya kujiandaa vizuri kwa mechi hiyo inayokuja.

TFF hii ndiyo itakayoendelea kupata sifa ya mafanikio ya Vilabu vyake.

TFF hii ndiyo itakayopata Sifa ya Mafanikio ya Ligi yake.

TFF hii ndiyo itakayoendelea kupata Sifa ya hapo baadae Vilabu kuongezeka kwenye ligi za CAF.

TFF hii ndiyo itakayoendelea kupata 10% ya kila fedha ambayo Simba itapata kwa kuvuka kila hatua na kuzitumia pesa hizo kwa maendeleo ya Soka Tanzania.

Fikiria kuanzia hatua ya Makundi TFF imepata zaidi ya Milioni 200 kupitia mafanikio ya Simba kutoka CAF.

Al Ahly walikuwa na viporo si chini ya saba.

JS Saoura, As Vita nao walikuwa na viporo si chini ya saba...tatizo liko wapi??..

Ni kweli TFF inataka kukwepa lawama za Viporo huku ikipoteza mambo muhimu kabisa kwa Taifa kuelekea mechi za CAF..??

TFF tafadhalini sana...Msichoke kuisaidia Simba kwa manufaa ya Taifa.

Haijalishi walisema walitaka kufika Robo Fainali ya Klabu Bingwa hivyo nanyi Mjitosheleze kuwa Inatosha kuipa nafasi Simba ya kujiandaa.

Lawama mnazozikimbia zinaweza kuwaandama maradufu.

Chiki Mchoma.
Fanani.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
ushawai kuona ligi gani mtu anafikisha viporo hadi mechi 10..
weka table za ligi za timu zote nane zilizofika robo fainali.. kisha tuone kama ligi za nchi nyingine zinaruhusu viporo.. kisa unacheza klab bingwa...
Ushawahi kuona ligi gani timu inacheza mechi nane nyumbani mfululizo?
 
TFF sasa hivi wanahangaika na taifa stars, simba pambaneni wenyewe kwanza hata mkijiandaa mwaka mzima hamuwezi kuwatoa tp mazembe
Hivi TFF inaweza kuhamasisha mashabiki wajae Kwa mkapa na wakafika hata mia tatu? TFF inaweza kuwapa fedha simba wakamsajili Zana coulbaly? Msaada wa TFF kwa vilabu unaufahamu?
 
ushawai kuona ligi gani mtu anafikisha viporo hadi mechi 10..

weka table za ligi za timu zote nane zilizofika robo fainali.. kisha tuone kama ligi za nchi nyingine zinaruhusu viporo.. kisa unacheza klab bingwa...
yaani mikia kabebwa huyo.
 
ushawai kuona ligi gani mtu anafikisha viporo hadi mechi 10..

weka table za ligi za timu zote nane zilizofika robo fainali.. kisha tuone kama ligi za nchi nyingine zinaruhusu viporo.. kisa unacheza klab bingwa...
Viporo vipo karibu ligi zote za Afrika,Haya ISMAILIA (MISRI)ana vipolo vingapi,na HUSSEIN DEY nae ana viporo vingapi(ALGERIA),fuatilia mpira acha porojo!!..
20190402_132020.jpeg
20190402_131929.jpeg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
badala ya kujibu swali unauliza swali.. mazembe ana viporo vingap, horoya ana viporo vingap, esperence ana viporo vingap, al ahly ana viporo vingap?
taja timu hata moja caf iliyomzidi simba kwa viporo
Hakuna mtani, sasa jibu na swali langu ni ligi gani duniani timu inaweza kucheza mechi nane nyumbani mfululizo?
 
Zamaleck anacheza kombe la Shirikisho caf na Al Ahly klabu bingwa .. halafu angalia hizo nchi kubwa kuna timu jumla ngapi katika ligi kuu.
 
Ligi kuu ya Misri ina timu 17,ya Morroco 16,ya Algeria 16 ya DRC Congo timu 16. Na kwetu timu ngapi? Halafu tutazame pia miundo mbinu ya nchi yetu n.k. halafu kumbuka ligi yetu haina mdhamini mwaka huu. Na mpira ni pesa.
 
TFF haijaionea simba. Ni wakati mzuri wa Kocha awatumie wachezaji wanaokaa sana benchi. Achanganye wale ambao hawakucheza mechi ya Mbao mbona ushindi upo. (Dida, Kwasi, Gyan, Mlipili, Juuko, Mzamiru, Niyonzima, Ndemla, Salamba, Okwi na Mo)
 
Back
Top Bottom