TFF Muionee huruma Lipuli FC

TFF Muionee huruma Lipuli FC

mnyikungu

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2009
Posts
1,962
Reaction score
2,477
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) mnapaswa kuionea huruma Lipuli Fc, timu hii inashiriki mashindano mawili yaani Ligi kuu na shirikisho lakini mara nyingi ratiba inazokutana nazo ni kama vile haya mashindano yanasimamiwa na vitu viwili tofauti na si TFF.

Mara ya kwanza makosa haya yalionekana mchezo wa nusu Fainali ambapo Lipuli ratiba ilionyesha anatakiwa aende mkoa wa Mara tarehe 3/5/2019 kisha Arudi Iringa kupambana na Yanga nusu fainali tarehe 6/5/2019 ambapo ni dhahili kabisa kwa uwezo wa club hii wasingeweza, lakini nadhani Lipuli waliomba basi angalau mchezo na Biashara Urudishwe Nyuma hadi tarehe 30/4/2019, wakati Lipuli inatoka Mkoani Mara mshindani wake Yanga alikuwa anatoka Mkoa wa mbeya tu ambapo ni masaa matano au sita kufika Iringa..hapo utaona nani anapata faida. Lipuli kabla ya kucheza na biashara Ilikaa wiki tatu bila kucheza hata Biashara nao hawakuwa na Mchezo wowote kwa muda mrefu ambapo kwa busara za TFF kama zingetumika na ukiangalia umuhimu wa nusu fainali ile basi mchezo ule ungepangwa mapema kabisa ili kuzipa timu shiriki muda wa kujiandaa.

Hayo yalikuwa ya nusu Fainali , sasa imekuja hii ya fainali yenyewe, kwa kawaida fainali ni jina kubwa na lenye hadhi, ukisikia fainali hata maandalizi yake lazima yawe makubwa, lakini kwa TFF fainali ya shirikisho haipewi umuhimu huo, Faibali timu zinatakiwa zipewe muda wa kujiandaa ili kuleta msisimuko na hadhi ya shirikisho lakini tofauti kabisa na fainali za shirikisho mwaka huu. Fainali za mwaka huu zitapigwa uwanja wa Ilulu mkoani Lindi na zitavikutanisha vilabu viwili vya Azam na Lipuli. Fainali hizi zitachezwa tarwhe 1/6/2019, hapa ndipo penye shida.

Michezo ya kumaliza ligi inachezwa tarwhe 28/5/2019 huku Azam akiwa mkoani Dar es Salaam na Lipuli atakuwa anakwaana na Prison mkoani mbeya, AZam atatumia masaa sita au saba huku Lipuli wakitumia zaidi ya masaa 18 kufika Lindi, hii inamaanisha Lipuli wamalize tarehe 28 kisha waondoke wakacheze tarehe 1 mwezi wa sita, ambapo kwa vyovyote file timu itafika tarehe 30 lindi kisha tarehe moja acheze mechi ya Fainali...hiki ni kituko na ni dhuruma kubwa kwa Lipuli, Azam yeye atafika huenda tarehe 28 usiku au tarehe 29 na atapata muda mzuri wa kujiandaa kuliko Lipuli ambayo haitapata huo muda.

Kwa vyovyote vile TFF muangalie namna gani Lipuli itapata ahueni na muda wa kujiandaa na hiyo mechi, Muifanye fainali hii iwe ya ushindani na yenye mvuto, kuliko kuacha ratiba hii ambayo ni dhahiri itaibeba AZAM
 
TFF timu pekee wanayoijali ni SIMBA. hizo nyingine sijui LIPULI hawana habari nazo. usishangae rais wa tff atahudhuria mechi ya kuwakaedhi simba kombe kesho lakin hiyo fainali huko lindi hatakuja! hii ndio tff
 
Lipuli wanatakiwa wajiongeze
Awamu ya kujilizaliza waachane nayo
Wakate tu mshiko vingenevyo wanaeza kupangiwa hata uwanja wa sumbawanga[emoji1321]‍♂️
 
TFF timu pekee wanayoijali ni SIMBA. hizo nyingine sijui LIPULI hawana habari nazo. usishangae rais wa tff atahudhuria mechi ya kuwakaedhi simba kombe kesho lakin hiyo fainali huko lindi hatakuja! hii ndio tff
Binafsi sioni upendeleo wowote zaidi ya ushamba wa Kuendesha soka. Huwezi kuwa na viongozi wasio na maono ukategemea maendeleo.
1.Timu inakaaje wiki 3 bila mechi utafikiri ligi imesimama kupisha majira ya baridi?
2.Timu itapewaje mapumziko wiki 3 bila mechi kisa inashiriki maahindano ya kimataifa?
3.Uliwahi kuona ligi gani duniani (Hata Ndondo) timu inakuwa na mechi 13 viporo?
4.Ni kawaida mechi ya ligi kuahirishwa timu ngeni imeshaondoka iko njiani.
5.Ratiba ya ligi inapangwa kwa kufuata "siasa" za Simba & Yanga.
6.Mchezaji aliyefanya kosa anaahirishiwa kutekeleza adhabu hadi mechi ya Simba na Yanga ipite ndo aanze.

Binafsi naona ushamba zaidi ya upendeleo. Usishangae mwakani Yanga akawa na Viporo kama vya Simba mwaka huu ili kubalance mzani.
 
Lipuli wana hoja hapa! Ila kwa namna wanavyotukamiaga acha wateseke! Wametuharibia sana msimu huu!
 
TFF timu pekee wanayoijali ni SIMBA. hizo nyingine sijui LIPULI hawana habari nazo. usishangae rais wa tff atahudhuria mechi ya kuwakaedhi simba kombe kesho lakin hiyo fainali huko lindi hatakuja! hii ndio tff
Simba wapi???...hao waliokuwa wanapumzika siku moja alafu kesho yake wanacheza mechi....simba anacheza tarehe 19 dar es salaam alafu tarehe 21 anamechi singida...hayo yote watu hawayaoni but kwa kuwa ni mashabiki wa yanga wamebakia kulia lia tu huku mitandaoni na kulalamika kuwa simba anabebwa
 
Wacha dawa iwaingie kitu walichotufanyia msimu huu ni halali kwa wanayowakuta,wao wabajua kuikamia yanga tu basi!
Sio kuikamia yanga tu...timu zote za ligi kuu zinapokutana na simba or yanga huwa zinakamia...na kufungwa kwenye mpira ni kawaida hata ukimleta barcelona aje acheze kwenye ligi yetu ingawa uhakika wa kuchukua ubingwa ni 100% but kuna mechi lazima atafungwa tu
 
Issue iko hivi sie lipuli kabla mechi ya tr28 first eleven yetu yote itakuwa tayari imefika lindi ila kwa usiri mkubwa huko mbeya tunaenda kuchezesha underdog na tunajua tutafungwa tu azam wajipange msimu ujao
 
Mchawi wa Mwafrika ni Mwafrika mwezie...hapo ndio tunategemea ukuaji wa soka.Hapana kwa kweli...tuna roho za ajabu sana sisi watu weusi
 
Nyinyi lipuli kama hamna nauli ya ndege ya kutoka mbeya, mtaweza wa fuata raja cassablanka Morocco uko.

Mwenzenu mtibwa alikosaga nauli
Nanyi mnataka mkibeba Kombe
Mtutie aibu tena
 
Binafsi sioni upendeleo wowote zaidi ya ushamba wa Kuendesha soka. Huwezi kuwa na viongozi wasio na maono ukategemea maendeleo.
1.Timu inakaaje wiki 3 bila mechi utafikiri ligi imesimama kupisha majira ya baridi?
2.Timu itapewaje mapumziko wiki 3 bila mechi kisa inashiriki maahindano ya kimataifa?
3.Uliwahi kuona ligi gani duniani (Hata Ndondo) timu inakuwa na mechi 13 viporo?
4.Ni kawaida mechi ya ligi kuahirishwa timu ngeni imeshaondoka iko njiani.
5.Ratiba ya ligi inapangwa kwa kufuata "siasa" za Simba & Yanga.
6.Mchezaji aliyefanya kosa anaahirishiwa kutekeleza adhabu hadi mechi ya Simba na Yanga ipite ndo aanze.

Binafsi naona ushamba zaidi ya upendeleo. Usishangae mwakani Yanga akawa na Viporo kama vya Simba mwaka huu ili kubalance mzani.

Umejadili vizuri ndugu, ni watu wachache wanaotazama mambo objectively kama wewe
 
Nyinyi lipuli kama hamna nauli ya ndege ya kutoka mbeya, mtaweza wa fuata raja cassablanka Morocco uko.

Mwenzenu mtibwa alikosaga nauli
Nanyi mnataka mkibeba Kombe
Mtutie aibu tena
Kwani kuna ndege za Mbeya Lindi?
 
Binafsi sioni upendeleo wowote zaidi ya ushamba wa Kuendesha soka. Huwezi kuwa na viongozi wasio na maono ukategemea maendeleo.
1.Timu inakaaje wiki 3 bila mechi utafikiri ligi imesimama kupisha majira ya baridi?
2.Timu itapewaje mapumziko wiki 3 bila mechi kisa inashiriki maahindano ya kimataifa?
3.Uliwahi kuona ligi gani duniani (Hata Ndondo) timu inakuwa na mechi 13 viporo?
4.Ni kawaida mechi ya ligi kuahirishwa timu ngeni imeshaondoka iko njiani.
5.Ratiba ya ligi inapangwa kwa kufuata "siasa" za Simba & Yanga.
6.Mchezaji aliyefanya kosa anaahirishiwa kutekeleza adhabu hadi mechi ya Simba na Yanga ipite ndo aanze.

Binafsi naona ushamba zaidi ya upendeleo. Usishangae mwakani Yanga akawa na Viporo kama vya Simba mwaka huu ili kubalance mzani.
Namba sita imechekesha na kunionyesha bado tunasafari ndefu sana, Ila mwisho umekubali kuwa ukiacha ushamba wa viongozi bado kuna timu mbili zinapendelewa sana
 
Siku tukitaka Mpira uendelee basi lazima tutoe upendeleo, mashindano ya Sport pesa yalisimamisha ligi kwanini mechi ya fainali ya shirikisho Timu zisipewe Muda wa kujiandaa?. Simba walikuwa mpaka wanaamua hii mechi hatuchezi au hii mechi tunacheza kwasababu ya kupisha maandalizi ya mechi za CAF....sasa kwanini Lipuli na Azam nao wasipewe muda wa kutosha kujiandaa na Fainali? Kwa hili najua mnataka Azam iwe bingwa bila shaka
 
Back
Top Bottom