mnyikungu
JF-Expert Member
- Jul 26, 2009
- 1,962
- 2,477
Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF) mnapaswa kuionea huruma Lipuli Fc, timu hii inashiriki mashindano mawili yaani Ligi kuu na shirikisho lakini mara nyingi ratiba inazokutana nazo ni kama vile haya mashindano yanasimamiwa na vitu viwili tofauti na si TFF.
Mara ya kwanza makosa haya yalionekana mchezo wa nusu Fainali ambapo Lipuli ratiba ilionyesha anatakiwa aende mkoa wa Mara tarehe 3/5/2019 kisha Arudi Iringa kupambana na Yanga nusu fainali tarehe 6/5/2019 ambapo ni dhahili kabisa kwa uwezo wa club hii wasingeweza, lakini nadhani Lipuli waliomba basi angalau mchezo na Biashara Urudishwe Nyuma hadi tarehe 30/4/2019, wakati Lipuli inatoka Mkoani Mara mshindani wake Yanga alikuwa anatoka Mkoa wa mbeya tu ambapo ni masaa matano au sita kufika Iringa..hapo utaona nani anapata faida. Lipuli kabla ya kucheza na biashara Ilikaa wiki tatu bila kucheza hata Biashara nao hawakuwa na Mchezo wowote kwa muda mrefu ambapo kwa busara za TFF kama zingetumika na ukiangalia umuhimu wa nusu fainali ile basi mchezo ule ungepangwa mapema kabisa ili kuzipa timu shiriki muda wa kujiandaa.
Hayo yalikuwa ya nusu Fainali , sasa imekuja hii ya fainali yenyewe, kwa kawaida fainali ni jina kubwa na lenye hadhi, ukisikia fainali hata maandalizi yake lazima yawe makubwa, lakini kwa TFF fainali ya shirikisho haipewi umuhimu huo, Faibali timu zinatakiwa zipewe muda wa kujiandaa ili kuleta msisimuko na hadhi ya shirikisho lakini tofauti kabisa na fainali za shirikisho mwaka huu. Fainali za mwaka huu zitapigwa uwanja wa Ilulu mkoani Lindi na zitavikutanisha vilabu viwili vya Azam na Lipuli. Fainali hizi zitachezwa tarwhe 1/6/2019, hapa ndipo penye shida.
Michezo ya kumaliza ligi inachezwa tarwhe 28/5/2019 huku Azam akiwa mkoani Dar es Salaam na Lipuli atakuwa anakwaana na Prison mkoani mbeya, AZam atatumia masaa sita au saba huku Lipuli wakitumia zaidi ya masaa 18 kufika Lindi, hii inamaanisha Lipuli wamalize tarehe 28 kisha waondoke wakacheze tarehe 1 mwezi wa sita, ambapo kwa vyovyote file timu itafika tarehe 30 lindi kisha tarehe moja acheze mechi ya Fainali...hiki ni kituko na ni dhuruma kubwa kwa Lipuli, Azam yeye atafika huenda tarehe 28 usiku au tarehe 29 na atapata muda mzuri wa kujiandaa kuliko Lipuli ambayo haitapata huo muda.
Kwa vyovyote vile TFF muangalie namna gani Lipuli itapata ahueni na muda wa kujiandaa na hiyo mechi, Muifanye fainali hii iwe ya ushindani na yenye mvuto, kuliko kuacha ratiba hii ambayo ni dhahiri itaibeba AZAM