Moshi25
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,555
- 4,118
Nimeangalia mchezaji wa Pamba mwamba kabisa kapiga goli la Maradona, katoka katikati ya uwanja kapiga chenga wachezaji wote wa Azam na kumalizia kumlamba chenga kipa wao na akafunga goli safi kabisa, maajabu ya dunia refa na kibendera wake wakakataa goli ukweli nikaona aibu sana nikaenda zangu mitaani kunywa kahawa. Mpira gani huu wa tiefutiefu mbona wanatuchosha hivi?Tazama mwamuzi anavyoinyonga Pamba jiji, kawanyima penati na goli.
Jana nimejua kumbe Azam pia ni big fish, kumbe sio Simba tu wanabebwa, hata Azam pia wanabebwa
Shime timu ndogo msikubali kuonewa muwe mnafungua madai itasaidia kupunguza uonevu