TFF na Bodi ya ligi inawakingia kifua marefa wanaochezesha hovyo kwa kuwapiga faini wakosoaji

TFF na Bodi ya ligi inawakingia kifua marefa wanaochezesha hovyo kwa kuwapiga faini wakosoaji

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
Nimeshangazwa na hii habari iliyoandikwa na ukurasa wa mtandao wa mwananchi kuona Ally kamwe kupigwa faini.

"Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe ametozwa faini ya Sh1 milioni kwa kosa la kumkejeli na kumdhalilisha mwamuzi wa mechi ya Singida Big Stars dhidi ya Simba kupitia mtandao wa kijamii.

"Baada ya kumalizika kwa mechi, Ali Kamwe aliweka chapisho katika ukurasa wake binafsi wa mtandao wa kijamii wa Instagram, ambalo lilikuwa na picha ya mwamuzi (Malogo) huku akiunganisha na wimbo wa msanii wa muziki kizazi kipya, Billnass uitwao Maokoto, hali iliyoleta tafsiri ya kumhusisha mwamuzi huyo na masuala ya fedha ama rushwa," imeeleza taarifa ya Bodi ya Ligi"

Kama TFF na Bodi ya ligi inawapiga faini wakosoaji je hao marefa wanapewa adhabu gani kwa utumbo wanaoufanya uwanjani?

Kama hatutaona kufungiwa au faini kwa marefa waliochezesha mechi ya Dodoma fc vs Azam Fc na Refa Tatu Malogo aliyechezesha mechi ya Singida fountain Gate Fc dhidi ya Simba sc Basi tulio welevu kama NALIA NGWENA tutajua kuwa TFF na Bodi ya ligi inahusika kwa asilimia Mia kuwatuma marefa wachezeshe kwa maelekezo maalumu.
 
Saa ingine TFF wanajidhalilisha sana

Na huu utumbo wa marefa hautakaa uishe kwa mtindo huu. Zile mechi kila kitu kilikuwa wazi kabisa

Anyways njooni mnifungie na mimi sasa nasema MAREFA HASA WA KIKE HASA HASA YULE TATU KILA MECHI YA SIMBA ANABORONGA KWA KUIPENDELEA WAZIWAZI
 
Yaani nisiweke wimbo 'maokoto' na picha ya mwamuzi basi mniadhibu!?..hiyo tafsiri wametumia kamusi gani!?
 
Kuna hisia za Rushwa za Ngono, Duniani kote refa aliye vurunda mechi zaidi ya moja tena akionekana maamuzi yake yakiegemea timuiyoiyo inayo lalamikiwa kufaidika na uchezeshani wake usimamishwa.

Mpira si wa Tff wala kamati ya Marefa, wanatakiwa wasikilize na kufanyia kazi malalamiko ya mashabiki wa soka.

Ni kweli kwenye maamuzi kuna shida hasa awa wa kike, zipo tuhuma za rushwa za Ngono ndio maana ata waki vurunda awa wajibishwi.
 
Nikawaida Simba ikiongoza ligi kasoro za ligi ya bongo kuanza kuonekana
:Ukimtoa kikwete na baba ake manara mashabiki wa Yanga wote waliobaki hawana akili".

Mwaka jana Uto na Geita mtu kashika nje ya penat box wanaweka tuta mwaka jana hawakusema mpaka wamechukuwa ubingwa.

Ally kamwe toka alivyoenda uto nae kawa hamnazo huyu sio ndio aliomwita Mgunda Anfazi halafu ndio maana ulaya wanaweka VAR wanajua mambo kama hayo
 
WAMEMUADHIBU ALIYECHEZESHA MECHI YA DODOMA VS AZAM NA KUMUACHA ALIYECHEZESHA MECHI YA SINGIDA VS SIMBA.
IMG-20231019-WA0019.jpg
 
:Ukimtoa kikwete na baba ake manara mashabiki wa Yanga wote waliobaki hawana akili"
Mwaka jana Uto na Geita mtu kashika nje ya penat box wanaweka tuta mwaka jana hawakusema mpk wamechukuwa ubingwa hiyo Ally kamwe toka alivyoenda uto nae kawq hamnazo huyu sio ndio aliomwita Mgunda Anfazi halafu ndio maana ulaya wanaweka VAR wanajua mambo kama hayo
RAGE ALISEMA "MASHABIKI WA SIMBA NI MBUMBUMBU"

HUU UZI HAUJAKAA KIUSHABIKI KAMA WEWE UNAVYOLETA USHABIKI NA NDIYO MAANA NIKAANDIKA AZAM WALIHUJUMIWA.

KAMA ULITAZAMA MPIRA GOLI WALILONYIMWA SINGIDA NI HALALI LAKINI JE UNADHANI KWA MPIRA HUU TUTAPIGA HATUA.
 
YANGA ILIPEWA PENATI UNAKUMBUKA SIMBA WALIFUNGA GOLI KWA MPIRA ULIORUDISHWA KUTOKA NJE YA UWANJA.
Ni sawa lakini msimu huu ulipoanza wakati Yanga mmeanza kuwagonga watu goli tano tano mbona hamkulalama,mpaka Simba kuwa kileleni ndio mnaanza mayowe?
 
Back
Top Bottom