Tate Mkuu
JF-Expert Member
- Jan 24, 2019
- 33,092
- 96,127
Nimetoka kuangalia mechi ya mtoano, Kombe la Shirikisho la Azam muda si mrefu kati ya Tanzania Prisons vs Polisi Tanzania, na ambako Polisi Tanzania wamefanikiwa kusonga mbele kwa ushindi wa goli 2 kwa 0 dhidi ya Tanzania Prisons.
Kiukweli uwanja umeharibika vibaya kiasi cha kudhani labda wachezaji wanacheza kwenye jaruba la kupandia mpunga (kwa wakulima wa zao la mpunga watanielewa).
Ni aibu uwanja kama huu kuendelea kutumika ukiwa katika mazingira mabovu kiasi hiki! Na pia ni aibu kwa Serikali kuendelea kuruhusu CCM kuvimiliki hivi viwanja kinyume kabisa na matakwa ya Watanzania tulio wengi, huku ikishindwa kuviboresha! Badala yake inakusanya tu mapato, na kuyatumia katika matumizi yao binafsi!
Nashauri viwanja vyote ambavyo CCM imevikwapua baada ya Nchi kuingia kwenye mfumo wa Vyama Vingi, virudishwe kwenye Halmashauri zetu! Ili viweze kuendelezwa kwa manufaa ya Watanzania wote.