TFF naombeni sababu ya Kimantiki kwanini Mechi za Vilabu vya Simba na Yanga mmezibadilisha

TFF naombeni sababu ya Kimantiki kwanini Mechi za Vilabu vya Simba na Yanga mmezibadilisha

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Ratiba iliyokuwepo ilikuwa Weekend hii Simba SC icheze na Mbeya City FC na Yanga SC wacheze na Ihefu FC.

Mmeibadilisha juu kwa juu hii Ratiba na sasa Simba SC itacheza na Dodoma Jiji FC na Yanga SC nao watacheza nadhani na Ruvu Shooting FC.

Hivi TFF ni kwanini mnapenda mno Kuvibeba, Kuvilinda na Kuvidekeza hivi Vilabu Vikongwe Viwili vya Simba na Yanga?

Sasa mbona pamoja na Kuvibeba kote huku kila Siku hakuna wanachokifanya Kimataifa huku Mmoja akiwa na DNA ya kuishia Robo Fainali tu ya CAFCL na Mwingine akiwa na DNA ya kuishia hatua za awali na Kufungwa Magoli mengi?

Na huu Upuuzi wenu haujaishia tu hapa kwani hata katika Kuchagua Wachezaji wa Taifa Stars Kipaumbele chenu ni Kujaza Kwanza Wachezaji wengi wa Simba na Yanga kisha wa Vilabu vingine mnafanya Kujazilia tu.

Nachukia Simba na Yanga Kubebwa nanyi TFF na ndiyo maana Soka letu lipo pale pale tu na linadema dema Kutwa.
 
Ungeiweka ratiba iliyotoka kabla ya msimu kuanza halafu tulinganishe
 
Ratiba ya Ligi sio kuwa inapangwa na bodi ya ligi, chombo chenye maamuzi huru?
 
Kama kumbukumbu zangu haziko vibaya, Yanga alitakiwa kucheza na Ihefu Leo 29/09 na kisha Ruvu Oct 03. Simba alikuwa acheze na Mbeya City Sept 30 na kisha Dodoma J Oct 04.

Mechi za weekend hii zimeahirishwa sababu ya wachezaji wao kuwa Timu ya Taifa, yaani kina Muzamiru, Beno, Manula, Sure, Kibwana nk.
 
Ratiba ya Ligi sio kuwa inapangwa na bodi ya ligi, chombo chenye maamuzi huru?
Hakuna chombo kilicho huru pale TFF chini ya utawala wa Wallace Karia. Na huu ndiyo ukweli mchungu.

Na mimi naungana na myoa hoja. Sijaona sababu za msingi za kuahirishwa kwa hizo mechi za Yanga na Simba. Ligi ilitakiwa iendelee kama kawaida. Kuipekeka Taifa Stars Libya kwenda kucheza mechi mbili za kirafiki, yalikuwa ni maamuzi ya kijinga! Na yenye kila harufu ya upigaji.
 
Kabisa kabisa.....
 
Timu kupelekwa Libya kucheza mechi za kimataifa za kirafiki kwangu sioni tatizo, yale yalikuwa ni maamuzi kuendena na FIFA wanachotaka.

Tatizo ni kwanini wanahairisha mechi za Simba na Yanga zilizokuwa zichezwe weekend hii?

Huko duniani kote mechi za ligi zitachezwa kuanzia leo Ijumaa, kesho, na jumapili, sijui kwanini TFF bado wana kasumba ya kikoloni kuwapumzisha hao wachezaji wa Simba SC, na Yanga SC, pale wanapokaribia mechi za kimataifa.
 
Hapo wanaibeba timu yao pendwa Simba. wanabuy time Mgunda aandae kikosi.wameona aibu kuahirisha mechi ya Simba pekee.kikosi kipana Cha Yanga kipo tayari muda wowote ,wangekuwa na Nia njema na Yanga wangeharisha mechi ya Ruvu shooting ambayo iko imara na wanacheza siku chache kabla ya CAF champion ligue
 
Nadhani kwasababu team nyingi wachezaji wao wako katika majukumu ya national team kwa hyo wameweka mzani sawa ili kusiwepo na visingizio
 
Hakuna kitu kinachonikera kama kubadili ratiba pasi na sababu ya msingi
Hakuna chombo kilicho huru pale TFF chini ya utawala wa Wallace Karia. Na huu ndiyo ukweli mchungu.

Na mimi naungana na myoa hoja. Sijaona sababu za msingi za kuahirishwa kwa hizo mechi za Yanga na Simba. Ligi ilitakiwa iendelee kama kawaida. Kuipekeka Taifa Stars Libya kwenda kucheza mechi mbili za kirafiki, yalikuwa ni maamuzi ya kijinga! Na yenye kila harufu ya upigaji.
 
Bado Kuna kazi kweli naamini kabisa walemavu wa akili Ni wengi yaani mtu wa mpira kabisa anasema haoni sababu ya kupeleka timu Libya kucheza friend match
Kwani TFF wamejipangia Na wakati Ile calendar ya FIFA ndo inawataka wafanye hivyo
 
Huko duniani kote mechi za ligi zitachezwa kuanzia leo Ijumaa, kesho, na jumapili, sijui kwanini TFF bado wana kasumba ya kikoloni kuwapumzisha hao wachezaji wa Simba SC, na Yanga SC, pale wanapokaribia mechi za kimataifa

Ni kweli nchi zingine wachezaji wapo kwenye match fitness muda wote kwani wanacheza mechi zote za ushindani kwa kufuata ratiba ya ligi, kimataifa, ngao ya jamii, pre-season.

Huku kwetu kwanza wachezaji ni wavivu, mazoezi kwa kuvizia, lishe duni isiyo ya mwanamichezo, asilimia 40% umri mkubwa wamechoka hivyo lazima watafute namna ya kutegea mechi ila inatu cost timu za vilabu na ya taifa wanapokwenda kushiriki Champions league, Confederation Cup uchovu wa umri mkubwa wanakata pumzi.
 
Back
Top Bottom