TFF: Tunaendelea kupambana kuhakikisha Bernard Kamungo anaitumikia Tanzania

TFF: Tunaendelea kupambana kuhakikisha Bernard Kamungo anaitumikia Tanzania

Vile ukitaka passport wao ndio wanakuwa wa kwanza kuweka vikwazo,ukianza kutoboa shobo zinaanza,
 
Andaeni mikakati ya kuzalisha vipaji vya kutosha na siyo kung'ang'ani mchezaji mmoja kwenye taifa lenye raia mil. 61
 
Mwacheni kijana atengeneze pesa huko.

Mbona mna roho mbaya hivi? Nyie mtampa nini hapa?

Mngeanza kwanza kuwafanyia mema wachezaji waliopo hapa ili maisha yao yanyanyuke.
Mbona wachezaji wa kibongo wanapata posho nzuri wakichezea timu kibwa za bongo! Mfano feisal analipwa milioni 16 kwa mwezi.

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Serikali ya CCM iruhusu uraia pacha. Tunapoteza fursa nyingi katika nyanja za kiuchumi, michezo, nk kwa sababu tu ya kuendekeza misimamo yao ya kizamani.
 
Kwani TFF hawajui kama wanapambana na sheria za nchi?

Mpaka sasa Kamungo ni raia wa USA.

TFF wawe makini kuhusu huyu mchezaji kwa sababu itasababisha watu wamtolee macho na kufukunyua vifungu vya sheria ili kubaini uhalali wa uraia wake. Huyu ni tofauti na stori tunazosikia kuwa watoto wa wanasiasa wengine wana uraia pacha kisiri lakini, huyu mchezaji atakuwa ni mtu maarufu hivyo atafuatiliwa.

Ili awe raia wa Tanzania ni lazima aukane uraia wa USA kwa sababu Tanzania hatuna uraia pacha.
 
Shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF) limesema bado linaendelea na harakati za kuhakikisha Benard Kamungo anaitumikia Tanzania kwenye michuano mbalimbali

Mkurugenzi wa ufundi wa TFF amesema hata kama Benard Kamungo atacheza timu ya Taifa ya Marekani chini ya umri wa miaka 23 kwenye michuano ya Olimpiki 2024 bado atakuwa na nafasi ya kuitumikia timu ya wakubwa ya Tanzania (Taifa Stars) kama ambavyo baadhi ya wachezaji nyota wengi wamewahi kufanya kwenye mataifa mbalimbali ulimwenguni

View attachment 2777167
Hakuna haja ya kupambana, dawa ni katiba kuwa kama ya Kenya inayosema kuwa mtu yeyote aliyezaliwa Tanzania ni raia wa Tanzania hata akihamia nchi nyingine na kuchukua uraia wa huko alikohamia. Marekani ina wakenya wengi ambao ni raia wa marekani lakini bado ni wakenya na wanaitumikia kenya kwenye mambo ya kimataifa, lakini Tanzania kuna watu wa ajabu sana ambao wanaamua kuwatupilia mbali ndugu zao eti kwa sababu wamechukua uraia wa nje bila hata kujua mazingira yaliyopelekea ndugu zao hao wakachukua uraia huo wa nje.
 
Tff walikuwa usingizi
gani Mpaka kijana akaamua kuchezea u23 ya usa ? Au walikuwa hawamjui Mpaka juzi alivyocheza dhidi ya timu ya Messi wakaamka usingizini ? Walitaka kijana awabembeleze ?
Tff wanamjua na alishawahi kuitwa Taifa stars Ila hakucheza sababu hazijulikani labda huko Tff ndani wanajua.
 
Tff walikuwa usingizi
gani Mpaka kijana akaamua kuchezea u23 ya usa ? Au walikuwa hawamjui Mpaka juzi alivyocheza dhidi ya timu ya Messi wakaamka usingizini ? Walitaka kijana awabembeleze ?
Tff imelala tena usingizi wa pono kwenye suala la kuandaa afcon match za ufunguzi na fainali kenya wakiwa hata uwanja wa maana hawana wameanza kuleta fitna wao ndio waandae hizo match ikiwa TZ ndio imechangia kwa kiasi kikubwa kufanikisha afcon 2027 kuja kuchezwa ukanda huu
 
Back
Top Bottom