TFF tusomeeni upesi sana hiyo barua iliyofika mchana huu kwa DHL ili Wanasimba tujimwage mitaani

TFF tusomeeni upesi sana hiyo barua iliyofika mchana huu kwa DHL ili Wanasimba tujimwage mitaani

Status
Not open for further replies.
Kwa habari za chini ya Kapeti ambazo bado naendelea kuzihakiki zinasema kwamba hatimaye tayari FIFA wameshafanya maamuzi juu ya Rufaa ya Simba SC na kwamba kuna barua imeshatumwa tena kwa DHL kwenda TFF ikiwa na maamuzi kuwa Simba SC ndiyo washindi wa rufaa yao na kwamba zile points 3 walizopewa na Kamati ya Saa 72 ni halali ila TFF wanaogopa kutangaza kwa kuhofia pengine fujo zitatoteka.

Ewe Mwanasimba SC popote ulipo kuanzia muda huu anza sasa kujiandaa kwenda mitaani kushangilia kwani sasa ni rasmi kuwa Simba SC ndiyo Bingwa wa VPL na muda wowote TFF watatangaza.

Hongereni sana Uongozi wa Simba SC na hasa Mzee wetu Ismail Aden Rage kwa kuipigania haki ya Simba SC ambayo hatimaye kupitia TFF leo tumeipata na sasa Wanasimba tunaanza kujiandaa kusheherekea Ubingwa.

Mwanasimba yoyote upatapo tu taarifa hii mtaarifu na mwanasimba mwenzio na anzeni sasa kufanya mazoezi ya kuushangilia Ubingwa ambao ni haki yetu na tumeuhangaikia kwa muda mrefu. Na kama kuna Mtu aliye karibu hapo na Msemaji wa TFF Bwana Alfred Lucas tafadhali mwambieni awaite Press ( Wana Habari ) na atangaze kilichopo katika hiyo barua iliyowafikia kwa njia ya DHL mchana huu.

Leo nina furaha ya ajabu kwanza......

  1. Liverpool FC tumeingia nne bora
  2. Serengeti Boys jana imeyaaga mashindano huko Gabon
  3. Simba SC imepewa haki yake na FIFA na Simba SC sasa ndiyo mshindi rasmi wa VPL.
Wana Yanga FC wote duniani pote poleni sana na sasa mnaweza tu kwenda kushangilia na wale Vyura wenu mnaowafuga pale Uwanjani Kaunda ila taarifa iwafikieni kuwa FIFA wameipa Simba SC ushindi na tuleteeni upesi sana Kombe letu kabla hatujalifuata wenyewe.
Mkuu Genta, hujawahi kuniangusha, hope na hii habari ni genuine!
 
Fifa watataka taarifa ya marefarii wa mechi tatu za kadi za njano za Fakhi. TFF itaanza kusema Simba walichelewa kulipia ada. Fifa itasema leta cheti baba, maneno mengi ya nini? TFF itanywea na kupeleka taarifa za marefarii. Hapo kitakachofuata sijui ni nini ...
 
Mkuu Genta, hujawahi kuniangusha, hope na hii habari ni genuine!
Mkuu nivizuri ukatumia akili kidogo tu kwani FIFA kamwe hawawezi kufanya maamuzi bila ya kuwashirikisha wanachama wao ambao ni FA ya nchi husika
 
IMG_3445.jpg

Barua yetu ilikua na uzito wa 1.50 Kg naomba nijue majibu ya FIFA yamefika angalau 2kg ili angalau nipate matumaini sisi mikia tumepata za mezani.
 
mtoa habari anaseme ni habari chini ya kapeti kuwa barua imefika kisha anadai wapewe ubingwa kipi ulicho ambiwa kuhusu hiyo barua
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom