TFF, vazi nadhifu ni lipi?

Write your reply...nimenote kitu hapa.. kuna mambo uongoz wa TFF uliyatarajia na hayajatokea na yamesababisha mparanganyiko wa mambo.. UD Songo mmeacha zahma
 

Ukivaa kama Mpoto huna nidhamu?

Zahera angekuwa Mmasai na kuvaa kimasai asingekuwa na nidhamu?

Ukivaa kigogo ni vibaya?

Ukivaa kaptula ni vibaya?

Vazi la TFF ni lipi?

Kwanini wachezaji na waamuzi wa kike wavalishwe bukta kama nia ni kulinda heshima na nidhamu?

Kwani malengo hasa ya kuvaa ni nini? Hili litasababisha nusu ya wapenda soka nchini wauchukie uongozi wa TFF hadharani
 
Yani nyie Yanga kwa upumbavu wenu ndo mtaichukia TFF.
Ila kanuni imetangazwa kabla hata ligi haijaanza, kama mgekua na akili msingekua mnalalamika baada ya Zahera kupigwa faini, mgelalamika pale tu TFF wametangaza hiyo sheria.
Kutokujua kitu gani kitatokea badae nao pia ni ujinga.
Huyo Zahera alisikia kabsa kuhusu hiyo sheria lakini kwa kiburi cha kujifanya ka yeye ndo anajua sana kuliko wengine kamua kuvaa hivyo hivyo.
Huyu Zahera anajua kabsa kuna sheria kutokubwatuka bwatuka lakini akaendelea kubwatuka bwatuka tu.
Nyie Yanga na Wandishi wote wa habari za michezo kwa upumbavu wenu ili jambo angepigwa faini kocha wa timu nyingne tofauti na Simba na Yanga hii isingekua habari.
Lakini kwa sababu wa uvivu wa kutafuta habari mmebaki mnajadili hili jambo wakati Kwenye sheria lipo.
Mgeonekana watu wenye akili ka hili jambo mgelijadili wakati TFF wanatangaza mabadiliko ya sheria sio baada ya kuanza kutekeleza.
Ona sasa lile goli walilonyimwa Ruvu shouting haikua habari sana kwa sababu ilikua inaifavour timu ambazo ndo mnaita timu kubwa.
Acheni ushamba fikiria jambo kwa ukubwa sio kuuachia ushabiki ufikirie.
 
Duh! wewe ndo hamnazo kabisa!!!

Zahera kusema ratiba mmeipanga vibaya kuruhusu timu moja kuwa na viporo 20 nyuma ya timu zote ni kubwatuka? Zahera kusema Simba ingepaswa ianze kucheza mechi ya ligi kabla ya Yanga kwakuwa wao hawakuhitaji kusafiri ni kubwatuka?

Zahera kusema waamuzi wanapendelea ni kubwatuka?

TFF ilishindwa nini kufafanua maana ya vazi nadhifu na heshima? Je, vazi la heshima ni vazi lenye nembo ya club?, Heshima kwa nani, watazamaji? mdhamini? TFF? watoto? au kwa nani hasa?.

Je, wakinadada zetu na waamuzi ya kike kuvaa bukta uwanjani ndiyo maadili yetu watanzania au ni unadhifu? Sisi wadau wenu wa michezo tunashindwa kukueleweni mlilenga nini kuiweka kanuni ile pale. Kanuni hii inaji contract na ni ambiguous kwelikweli kwakuwa haionyeshi manufaa yake na malengo yake kwenye mchezo mzima wa mpira wa miguu. Hasa kutokana na kwamba pale uwanjani kuna wachezaji, waamuzi, makocha na watatazamaji mabibi na mabwana, watoto na wakubwa waliovaa kaptula na t-shirts pia. Sasa hiyo heshima inayoletwa na uvaaji iko wapi?

Kwavyovyote vile Zahera ni kocha mkubwa hapa nchini, labda kama mdhamini anapenda asaidie kuitangaza vizuri brand yake kwa namna fulani ya kuvaa, kama ni hivyo basi mdhamini hana budi kufanya makubaliano mapya na Zahera na Yanga, au Aussems na Simba (timu kubwa nchini) namna gani wataweza kuitangaza vema brand ya mdhamini kwa makubaliano fulani. Lakini mdhamini asitegemee the same millage ya brand yake kupitia kwa Aussems, Zahera, Matola, Mayanga, Minziro, Mexime, Simba, Yanga, mtimbwa, Namungo, Ruvu nk.

Hawa watu na hizi timu zina hadhi na thamani tofauti kabisa. Unapotaka Patrick Aussems avae shati linaloitangaza vodacom bei yake sio sawa na Mexime au Nsajigwa wanapovaa shati la aina hiyohiyo. Yanga, Simba, Azam lazima wawe na vifurushi tofauti na Namungo. Hivyo mdhamini na TFF hana budi kuzungumza na hawa super coaches na super teams (Yanga, Simba, Azam) kuhusu namna ya kuvaa, kujiheshimu na malipo badala ya kusema jumlajumla mavazi nadhifu na heshima.

Zahera anaweza kuendelea kuvaa kaptula zake zilezile lakini zilizowekewa nembo ya Yanga kwenye paja utamwambia nini?
 
Huyo Raia wa Somalia wamrudishe kwao kabla hatujamchoma mtoto!
 
TFF wanafanya ubaguzi, eti Zahera hakuvaa nadhifu huku kocha wa Simba akiachwa amevaa shati la mtumba alilonunua Karume.
 
Ni kweli kabisa mfano mechi ya Ruvu na Yanga ilitakiwa iwe 2-0 line woman akagoma, hawa ndio wanauwa soka letu.
 
Umenena kweli, wapo kimya hawaongelei goli la 2 la Ruvu Shooting, double standards, mkuki umegeukia kwao wamegundua kumbe unachoma.
 
Sasa nyie gongowazi si mkubali tu makosa ya mwl wa timu yenu?!!!
Lile lijamaa lilikosea siku ile, cha kufanya mngeongea naye na kufanya mikakati ya timu yenu kuangalia namna timu yenu itacheza bila mwalimu kuwepo katika benchi la ufundi..
Zahera ana dalili ya dharau ndio mana alijikalia kwao weeee na kusahau kuwahi kuja kupanga timu yake na maandalizi ya ligi!..
.
.
Nawashauri liangalieni hili pia ikiwezekana mmkanye na kumpa utaratibu kulialia kwenu haukusaidii
 
Jamaa wanalialia tu badala ya kukaa na mwl wao waweke mikakati ya timu kucheza bila mwl
Umenena kweli, wapo kimya hawaongelei goli la 2 la Ruvu Shooting, double standards, mkuki umegeukia kwao wamegundua kumbe unachoma.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…