TFF, vazi nadhifu ni lipi?

TFF, vazi nadhifu ni lipi?

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Vazi nadhifu Kwa mmasai linaweza lisiwe nadhifu Kwa Mchagga. Kama hakuna juhudi ya kutoa fafsiri ya maana ya vazi nadhifu hakutakuwepo na tafsiri moja ya vazi nadhifu.
Askali wa kikoloni walikuwa wanavaa kaptula, je hawakuwa nadhifu?

Kocha Mwinyi Zahera kapewa adhabu na tff eti Kwa kosa la kutovaa nadhifu, yaani kavaa kaptula na t-shirt ya pollo.

Adhabu kama hii inalitia aibu taifa na shilikisho.

Tff toeni maelezo/description ya nini maana ya vazi nadhifu ili muondoshe subjectivity kwenye kanuni yenu, vinginevyo Zahera ana haki ya kukata rufaa.
 
Mbaya zaid kocha wa ruvu naye alivaa pensi
Ninamuonaga guadiola akiwa amevaa vivazi wakati wa mechi. Kama chocha anatakiwa avae suti isemwe wazi kuwa kama kocha hatavaa jezi za club basi avae suti na tai na viatu vya ngozi na mkanda na soksi. Suti lazima ipigwe pasi. Maana unaweza kuvaa suti lakini hauko nadhifu.

Anavyovaa Patrick Aussens kocha wa Simba kwangu mimi namuona hajavaa nadhifu, lile jeans na shati jeupe ambalo hajalichomekea akiruka kushangilia goli tumbo lote liko nje Mimi naona kama hajavaa nadhifu.
 
Huu ni upuuzi mwingine wa Tifu tifu ka Keria.
 
Stress za kutolewa na ud songo bado zinawaandama tff ,huyo kocha wa azam walipocheza ngao ya jamii juzi kati,tena kipindi washatangaza hiyo sheria
IMG-20190903-WA0017.jpeg
 
Ninamuonaga guadiola akiwa amevaa vivazi wakati wa mechi. Kama chocha anatakiwa avae suti isemwe wazi kuwa kama kocha hatavaa jezi za club basi avae suti na tai na viatu vya ngozi na mkanda na soksi. Suti lazima ipigwe pasi. Maana unaweza kuvaa suti lakini hauko nadhifu.

Anavyovaa Patrick Aussens kocha wa Simba kwangu mimi namuona hajavaa nadhifu, lile jeans na shati jeupe ambalo hajalichomekea akiruka kushangilia goli tumbo lote liko nje Mimi naona kama hajavaa nadhifu.
Na makocha km pep ana mkataba na designer wake anavaa anavyojua yy

Km wana kisasi na huyo kocha waseme tu
 
Kwani Kingetokea nini endapo Zahera angebadili mavazi yake kuvaa kwa kadri dress code inavyotaka??Sheria imetoka na amekaidi??ukienda kinyume na sheria nini kifuate??

Upande wa Pili, Aussems alivaaje siku Simba inacheza na JKT Tanzania??

Kuna ambae ana kipengele hiko cha sheria ya uvaaji akiweke hapa tukidadavue??
 
Ndio maana soka letu limedumaa viongozi wanahangaika na vitu visivyo na msaada katika kukuza kandanda letu.

Waafrika ukiwa msema kweli lazima wakuadhibu kwa makosa ya kishenzi.
Sasa napata picha kwanini wakati wa uchaguzi wakinaJulio waliingia nakaulimbiu ya kutaka mpira wao. Yaan Zahera kuwaeleza ukweli Tff wamekuja na Kanuni za kumdhibiti. Kwasasa kama nchi hatunawa kumlaumu makosa tunayafanya sisi wenyewe wakatiwa wa kuchagua viongozi.
Tunachoweza fanyani kuvizia siku viongoz wote wa Tff wapo pale Karume na Mashabiki wa soka kuingia kwa nguvu na kutandika bakora viongozi wote na kuwafungia na makufuli mle ndani ujumbe utakuaumefika.
 
Kwani Kingetokea nini endapo Zahera angebadili mavazi yake kuvaa kwa kadri dress code inavyotaka??Sheria imetoka na amekaidi??ukienda kinyume na sheria nini kifuate??

Upande wa Pili, Aussems alivaaje siku Simba inacheza na JKT Tanzania??

Kuna ambae ana kipengele hiko cha sheria ya uvaaji akiweke hapa tukidadavue??
Nani akuwekee hicho kipengele wakati unasema sheria ilitoka na Zahera amekaidi? Si ukiweke wewe mwenyewe kisha ukitafsiri hapa?
 
Soka la bongo ni la kishenzi sana wanadeal na masheria mengi wameshidwa kukuza soka la uwanjani pumbav sana
 
Tff toeni maelezo/description ya nini maana ya vazi nadhifu ili muondoshe subjectivity kwenye kanuni yenu, vinginevyo Zahera ana haki ya kukata rufaa.
Kanuni specific kila klabu inazo, maana kila klabu ina mjumbe katika Bodi ya Ligi. Labda useme kwa faida yako wewe na washangiliaji wengine, ila vilabu vilishapewa na hata Zahera alijibu kuhusu kanuni hiyo kabla ya mechi hii ya Ruvu, ila akafanya makusudi

1567575423873.png
 
Back
Top Bottom