TFF, vazi nadhifu ni lipi?

TFF, vazi nadhifu ni lipi?

Ndugu yangu hawana kisasi na Mwl tu. Wanakisasi hadi na Yanga eti kisa UD Songo!
Labda pengine hujui kuwa miongoni mwa wanaotunga kanuni hizo, yupo kiongozi wa klabu ya Yanga, achilia mbali viongozi wa vilabu vingine wapenzi wa Yanga
 
Huyu jamaa sijui mchawi nataman nitukane tff Ila naogopa burn jf napapenda mno
Ila ni useng.e
 
Zahera ameadhibiwa kwa makosa mawili la kwanza ni hili la kutovaa kwa unadhifu na kingine ni kutumia lugha ya kejeli kwa TFF.
 
Ndio maana soka letu limedumaa viongozi wanahangaika na vitu visivyo na msaada katika kukuza kandanda letu.

Waafrika ukiwa msema kweli lazima wakuadhibu kwa makosa ya kishenzi.
Yote anayoyasema na kuyafanya Zahera ni yale yote yanayolikuza soka letu nchini. Mfano, Simba inapomsajili Kakolonya aliyeonyesha utovu wa nidhamu Yanga na Kwa coach ni kudidimiza nidhamu kwenye soka la Tanzania. TFF walitakiwa kumsaidia Kakolonya kupata haki zake Yanga bila kugomea kucheza mpira. Kwahiyo tff na Simba wameona kuwa Kakolonya alifanya vizuri kudai kwa kugoma kucheza mpira?

Zahera kusema ratiba ya vpl ni ovyo anadanganya? Na uhovyo huo ameutaja.

Zahera anaposema wachezeshaji wanaboronga anadanganya? Kama anadanganya mbona mashindano ya CAF hakukuwa na hata referee mmoja kutoka kwenye ligi yetu?

Tff iachane na mahaba ya timu moja, itaua mpira kwa kutaka kubeba baadhi ya timu migongoni mwao.

Viongozi wa club wasikae kimya.
 
Kanuni specific kila klabu inazo, maana kila klabu ina mjumbe katika Bodi ya Ligi. Labda useme kwa faida yako wewe na washangiliaji wengine, ila vilabu vilishapewa na hata Zahera alijibu kuhusu kanuni hiyo kabla ya mechi hii ya Ruvu, ila akafanya makusudi


View attachment 1197276
Kuwa smart ni kuwaje? It is a relative term. Tanzania haina dressing code, hivyo kila siku huwa wanatoa maelezo nini watu wasivae na nini kivaliwe wapi na lini.

Tff wasijifanye kuwa hawana weledi wa vitu vidogo kama hivi
 
Avae jezi za bench la ufund sio yale mapensi na matishet yake
Pensi na T-shirt siyo mavazi nadhifu? Umeshawahi ona ngoma ya mganda ya ndugu zetu wamanda ikichezwa? Umeshaona polisi wa enzi sile walikuwa wanavaa nini? Nadhifu ni nini? SUTI au?
 
Pensi na T-shirt siyo mavazi nadhifu? Umeshawahi ona ngoma ya mganda ya ndugu zetu wamanda ikichezwa? Umeshaona polisi wa enzi sile walikuwa wanavaa nini? Nadhifu ni nini? SUTI au?

Walioiandika hiyo kanuni ya uvaaji waliongozwa na chuki, hamaki, mhemko, hasira, jealous, hisia za kumlenga mtu mmoja wakasahau kuboresha walichokikusudia. Kanuni/sheria kama haiko FIFA, CAF wala CECAFA ni kanuni/sheria ya mtu badala ya mpira. Haifai kutekelezwa. ,

kwani makosha wanaenda kufunga ndoa pale uwanjani hadi wavae "nadhifu" sisi kule kwetu kuvaa nadhifu ni kuvaa shuka (mgolole) mweupe.
 
IMG_20190904_114849.png
 
Timu yao haipo kwenye yale mashindano mpaka Agosti, 2020! Wamepaniki.....
 
Labda wanatakiwa wachomekee mashati. Shuleni tulifundishwa kuwa usipochomekea shati huonekani uko smart. Hivyo kuchomekea shati ilikuwa sehemu ya sare ya shule. Hata zamani wachezaji walikuwa kitakiwa wacheze uwanjani wakiwa wamechomekea fulana zao kwenye bukta.

Nadhani kanuni ingeishia kusema makocha wavae nguo zenye rangi na nembo ya club zao ingeeleweka hata kama isingekuwa sawa kulazimishwa kuvaa nguo za club tu.
 
Vazi nadhifu Kwa mmasai linaweza lisiwe nadhifu Kwa Mchagga. Kama hakuna juhudi ya kutoa fafsiri ya maana ya vazi nadhifu hakutakuwepo na tafsiri moja ya vazi nadhifu.
Askali wa kikoloni walikuwa wanavaa kaptula, je hawakuwa nadhifu?
Kocha Mwinyi Zahera kapewa adhabu na tff eti Kwa kosa la kutovaa nadhifu, yaani kavaa kaptula na t-shirt ya pollo.
Adhabu kama hii inalitia aibu taifa na shilikisho.
Tff toeni maelezo/description ya nini maana ya vazi nadhifu ili muondoshe subjectivity kwenye kanuni yenu, vinginevyo Zahera ana haki ya kukata rufaa.
Leo timu ya taifa ivae suti uwanjani labda tutashinda
 
TFF na bodi ya ligi wote ni wapumbavu na mijitu ya hovyo kabisa
 
Back
Top Bottom