TFF waangalie huu upangaji wa Ratiba

Mtoto wa nzi

JF-Expert Member
Joined
Jun 6, 2012
Posts
10,017
Reaction score
18,537
Kwanza Mimi ni Yanga... Ila nikiangalia maelezo haya Kutoka app ya Mwana jangwani naona kabisa hawa Jamaa Kuna tatizo mahala...

Ratiba ya Yanga ya michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara kwa miezi ya tisa na kumi inaonyesha michezo yake yote huenda ikapigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Hii itakuwa ni nafasi nzuri kwa Yanga 'kujikusanyia' alama za kutosha kabla ya kuanza kuzunguuka mikoani.

Septemba 16 Yanga itaivaa Stand United kwenye uwanja wa Taifa ikiwa mwenyeji wa mchezo huo.

Siku tatu baadae, Septemba 19 Yanga itashuka tena uwanja wa Taifa kuivaa Coastal Union kisha Septemba 23 itashuka tena uwanjani hapo kuivaa Singida United.

Septemba 26 Yanga itakuwa ugenini dhidi ya JKT Tanzania mchezo huo pia utapigwa kwenye uwanja wa Taifa.

Septemba 30 itakuwa ugenini pia dhidi ya Simba, mchezo huo utapigwa uwanja wa Taifa.

Mwezi Oktoba ratiba inaonyesha michezo yote minne ya Yanga itapigwa jijini Dar es salaam

Oktoba 07 itacheza na Mbao FC kwenye uwanja wa Taifa wakati Oktoba 20 itacheza na Alliance katika uwanja huo huo.

Oktoba 25 itakuwa ugenini dhidi ya KMC mchezo ambao huenda ukapigwa kwenye uwanja wa Taifa isha kurejea tena dimbani hapo kuivaa Lipuli FC Oktoba 30.

Lakini pia Novemba 04 Yanga itashuka uwanja wa Taifa kuivaa Ndanda FC. Huku Novemba 07 ikitarajiwa kuwa ugenini kwenye uwanja huo au wa Uhuru kuivaa African Lyon

Hivyo kama ratiba haitakuwa na mabadiliko, huenda Yanga ikacheza michezo 11 mfululizo jijini Dar es salaam.
 
Mechi na JKT tungeweza kuwekwa tukaenda Mtwara na Ndanda, tukirudi TUNACHEZA na simba, tukitoka tunawafuata hao Alliance na Mbao, tunarudi kwa KMC Halafu Lipuli ,tukitoka tunaenda Kagera then Stand... hapo Kuna kuwa na wastani mzuri wa ratiba.
 
Kwahiyo game za SIMBA, KMC AFRICAN LYON, NA JKT Ulitaka zipigwe moro wakti umesema YANGA wako ugenini kwa hizo timu??? Hao wenyeji ndio watafute uwanja..
 
Hiyo Ratiba tu afu ubaya ni kwamba ligi yetu timu nyingi ziko dar... hata SIMBA akikutana na hizo timu atachezea dar...
 
Mwanzo gemu 3 za Ndala zilivyopangwa zote zichezwe ugenini.. Kelele zilisikika kila kona, Ndala wakilalamikia ratiba hiyo.. Leo mmejikuta mna gemu zaidi ya 9 nyumbani mnaanza kulalamika tena.. Mnataka ratiba iweje ili mridhike?
 
Mwanzo gemu 3 za Ndala zilivyopangwa zote zichezwe ugenini.. Kelele zilisikika kila kona, Ndala wakilalamikia ratiba hiyo.. Leo mmejikuta mna gemu zaidi ya 9 nyumbani mnaanza kulalamika tena.. Mnataka ratiba iweje ili mridhike?
Epl Kuna ARSENAL, CHELSEA, TOTTENHAM, CRYSTAL PALACE, FULHAM NA WEST HAM.... Lakini hauwezi kuta hata Mara moja eti timu ipo tu London Mechi 5 hata Kama za nyumbani na ugenini... Kuna tofauti gani na hizo timu za Dar AFRICAN KYON, KMC, SIMBA, YANGA,AZAM JKT TANZANIA timu sita vile vile Halafu timu icheze Mechi 11 hapo hapo mji mmoja... Ukiwa kichwa maji mwezi mchanga ngumu kuelewa hii concept
 
Sawa Kichwa Maziwa na Asali, Mwezi Uliokomaa, ambae umeweza kuielewa hii concept kirahisi.
 
Hupo sahihi kuikashfu ratiba ila unakosea kuilinganisha na EPL. Miundombinu na budget ndiyo ki kwazo hapa kwetu, hili limesha fafanuliwa sana na TFF.

NB: Msimu huu Yanga Mtashinda Njaa.
 
Sawa Kichwa Maziwa na Asali, Mwezi Uliokomaa, ambae umeweza kuielewa hii concept kirahisi.
njoo na point joooh... shombo sio mpango tunajenga ....mimi yanga.... Lakini Kuna yanga wanaifurahia... Lakini kispoti sio... Hata simba itawakuta hii mechi 6 sijui 7 nje... Hakuna upangaji wa hivi.... Ni uvivu wa TFF..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…