Mtoto wa nzi
JF-Expert Member
- Jun 6, 2012
- 10,017
- 18,537
Kwanza Mimi ni Yanga... Ila nikiangalia maelezo haya Kutoka app ya Mwana jangwani naona kabisa hawa Jamaa Kuna tatizo mahala...
Ratiba ya Yanga ya michezo ya ligi kuu ya Tanzania Bara kwa miezi ya tisa na kumi inaonyesha michezo yake yote huenda ikapigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Hii itakuwa ni nafasi nzuri kwa Yanga 'kujikusanyia' alama za kutosha kabla ya kuanza kuzunguuka mikoani.
Septemba 16 Yanga itaivaa Stand United kwenye uwanja wa Taifa ikiwa mwenyeji wa mchezo huo.
Siku tatu baadae, Septemba 19 Yanga itashuka tena uwanja wa Taifa kuivaa Coastal Union kisha Septemba 23 itashuka tena uwanjani hapo kuivaa Singida United.
Septemba 26 Yanga itakuwa ugenini dhidi ya JKT Tanzania mchezo huo pia utapigwa kwenye uwanja wa Taifa.
Septemba 30 itakuwa ugenini pia dhidi ya Simba, mchezo huo utapigwa uwanja wa Taifa.
Mwezi Oktoba ratiba inaonyesha michezo yote minne ya Yanga itapigwa jijini Dar es salaam
Oktoba 07 itacheza na Mbao FC kwenye uwanja wa Taifa wakati Oktoba 20 itacheza na Alliance katika uwanja huo huo.
Oktoba 25 itakuwa ugenini dhidi ya KMC mchezo ambao huenda ukapigwa kwenye uwanja wa Taifa isha kurejea tena dimbani hapo kuivaa Lipuli FC Oktoba 30.
Lakini pia Novemba 04 Yanga itashuka uwanja wa Taifa kuivaa Ndanda FC. Huku Novemba 07 ikitarajiwa kuwa ugenini kwenye uwanja huo au wa Uhuru kuivaa African Lyon
Hivyo kama ratiba haitakuwa na mabadiliko, huenda Yanga ikacheza michezo 11 mfululizo jijini Dar es salaam.