TFF wamjibu dogo aliyelalamika kulipwa 20,000

TFF wamjibu dogo aliyelalamika kulipwa 20,000

Kuna kipindi bosi wa Tanzania Farmers Association huwa anajisahau na kujikuta anatembea mitaanibakiwa ameshika kijiko.
Ile U-turn waliyoipiga TFF kutoka kwa Leodegar Chilla Tenga kwenda kwa huyu aliyepo, mpaka leo sikuwahi kuielewa kabisa.
na maadili ya uongozi hana kabisa. ashukuru upepo wa mafanikio ya Simba na Yanga umembeba.
 
Namuona Wallace Karia hapa kupitia Azam Sports 3 HD akijitutumua kujibu shutuma zilizoelekezwa kwake yeye na pia kundi lake la upigaji pale TFF. Ila bado hawezi kukwepa lawama. Posho ya elfu 20-50 kwa mtoto aliyeifanyia makubwa nchi yake, bado ni ubabaishaji.

Atuambie kwanza kama na wao wenyewe walipeana posho za elfu 20, au 50 kwa muda wote huo wa mashindano.
 
View attachment 2843785

nimeamka tu nimekutana na hii kutoka mwananchi. huyu ni dogo national team chini ya miaka 15, mashindano yamefanyika Uganda yameisha hivi karibuni. TFF wanadai wapo katika mchakato wa hundi. Vipi kuhusu mwaka jana kulipwa 50,000.

hii imenikumbusha ndugu yangu alichaguliwa national team beach soccer. Kambi TFF Karume aliishia kula tu na kupanda basi la TFF. Yaliyobaki tumwachie Mungu
Ukishaona wanaosaka kura wanatumia rushwa kuzipata elewa kuwa kwenye upmgozi wao hakuna jipya
 
TFF wamesema watajenga miundombinu, hawatagawa hizo pesa
Sawa, kujenga hiyo miundombinu ni maagizo ya huyo Motsepe kwa maelezo ya Wallace Kari!!

Tatizo liko kwenye hicho walichokifanya kwa hao watoto. Yaani wamepambana kwa jasho na damu mpaka wakafanikiwa wengine kuchukua ubingwa, na wengine kushika nafasi ya 3!

Je, ilikuwa ni sahihi kuwapa tu nauli ya elfu 20 ili warejee majumbani kwao? Ndiyo kusema hata hao viongozi waliowasimamia hao watoto hawakulipwa chochote? Au wamewachukulia kama viumbe visivuo na mahitaji yao binafsi?

Karia akubali kukosolewa! Na asijione yeye ndiyo mwenye akili kuliko binadamu wengine wote duniani.
 
Tanzania imepatiwa VAR ambayo itafungwa uwanja wa Benjamin Mkapa
 
Sawa, kujenga hiyo miundombinu ni maagizo ya huyo Motsepe kwa maelezo ya Wallace Kari!!

Tatizo liko kwenye hicho walichokifanya kwa hao watoto. Yaani wamepambana kwa jasho na damu mpaka wakafanikiwa wengine kuchukua ubingwa, na wengine kushika nafasi ya 3!

Je, ilikuwa ni sahihi kuwapa tu nauli ya elfu 20 ili warejee majumbani kwao? Ndiyo kusema hata hao viongozi waliowasimamia hao watoto hawakulipwa chochote? Au wamewachukulia kama viumbe visivuo na mahitaji yao binafsi?

Karia akubali kukosolewa! Na asijione yeye ndiyo mwenye akili kuliko binadamu wengine wote duniani.
kazi ya kujenga miundombinu ni ya serikali. ila zawadi za hao watoto kujengea miundombinu ni hujuma.
 
tff n matapelii hawamadogoodawaa n kuchomeshaaa kilamechii mama....
 
Back
Top Bottom