TFF wanaidekeza sana timu ya Simba kuliko Yanga

TFF wanaidekeza sana timu ya Simba kuliko Yanga

Mm sijajua simba wanawakataa mkataba wa gsm kwa kuwa hawakushirikishwa au wanaukataa mkataba kwa kuwa gsm ni wadhamin wa yanga pia?
 
Mtoa mada kwenye haya mambo ushabiki weka pemben alafu fuata sheria na kanuni ndo unaweza elewa kidogo bt kiukwel tiefuefu na gsm wake wamepuyanga kwa hili
Na ndiyo maana walijhami kwa kuweka zuio watu wasihoji chochote. Pumbavu kabisa wanamuendekeza Ghalib,huyu ni mtu wa chupli chupli maisha yake yote

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Gsm kama anataka kuwekeza awekeze Yanga,kama hataki atengeneze timu yake ipambane daraja la kwanza huko alaf iingie ligi kuu then ndiyo awavishe hao vijana wake hayo ma nembo yake kwa mbinu aliyotumia kwakwel amegonga mwamba simba saiz ina viongozi wenye upeo mkubwa
Usikute said gharib yey binafsi hana shida ila tatizo ni vilaza wanaomzunguka wanamshaur mambo ya ajab mwisho wake ni aibu na hasara kutengeneza mabango na kisha kuyabandika na kuyabandua kazi bure
Wadau wa yanga walikuwa wakifurah wakijua simba itavurugwa na vitu vidogo vidogo wamefeli..
Na Ghalib ni mnyama ila tu inapokuja kwenye kutafuta pesa anaangalia hela ilipolala ndiyo anapoamkia. Janjajanja.

Sent from my Nokia 5.1 Plus using JamiiForums mobile app
 
Kuhusu nembo ya NBC nadhani tff wali experience kwenye nembo ya gsm kuwa njano na kijani badala ya nyekundu na nyeupe.mwenye nembo akikubali rangi ibadilishwe akuna shida kikubwa ni nembo imevaliwa.
Hapa si suala la mdhamini kukubali bali kanuni za tff zinasemaje. Sheria haibadilishwi kiholela hivyo.

Kanuni inasema lazima nembo ya mdhamini ivaliwe mkono was bega la kulia na rangi zake.

Ni lini hii kanuni ilitenguliwa au kufanyiwa mabadiliko kisheria.

Tunatunga sheria na kuzikanyaga wenyewe kirahisi tu. Ni TZ tu mambo ya kijinga na kihuni km haya yanatokea.
 
Mpaka sasa hivi nje ya uwanja simba anaongoza goli mbili. Kesi ya morison cas na kukataa kuvaa nembo ya gsm
 
Kwasababu tajwa hapo juu na Simba nao wanadeka.
Jambo kama hili la mgogoro wa tff na Simba likitokea kwa Yanga uwa kuna press mfululizo za body ya ligi au tff kutoa vitisho na mikwara kwa Yanga.

Lakini kwa Simba tff na body ya ligi huwa wanaonyesha unyonge flani hivi tofauti na inavyotarajiwa.
Nawasilisha.
Hata nyumbani, mtoto mwenye kipato kikubwa na kuiletea familia heshima hupendelewa na hata mama yake anaweza kumuandalia maji ya kuoga.
 
Basi leo ndiyo siku ya Mechi ya Simba na yanga nikuambie usichojua basi unafikiri inakuaga mechi kali basi,
Mashabiki ndiyo huwa wanapania,wachezaji wao waala....maana wachezaji wanakuwa wameshachezeshwa na Maneno ya mashabiki,basi wanacheza masikio yapo juu..
Ila leo zamu ya #uto kulala mechi imeisha.
 
Back
Top Bottom