TFF wanatafuta kampuni moja ya ubashiri mechi ya Yanga na Simba ya Machi 1, 2026

TFF wanatafuta kampuni moja ya ubashiri mechi ya Yanga na Simba ya Machi 1, 2026

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
5,383
Reaction score
18,776
Hapa maana yake ni kwamba hakuna kampuni ya betting itaruhusiwa kuweka mchezo wa Simba na Yanga bila idhini ama kibali kutoka TFF, ambapo wao watamuuzia mtu mmoja tu na wengine wote wanapaswa kwenda kununua kwa aliyeuziwa haki za mchezo huo husika.

====

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) (TFF) linatafuta kampuni moja kwa ajili ya haki za kipekee za ubashiri (exclusive betting rights) katika mechi ya Yanga na Simba.

Mechi hiyo ya Ligi Kuu ya NBC itachezwa tarehe 1 Machi 2026 katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar kuanzia saa 2.15 usiku.

Wadau wote wa michezo ya kubashiri wanakumbushwa kuwa haki zote za Ligi Kuu ya NBC ni mali ya TFF na washirika wake (partners).

Kutokana na taarifa hii, kampuni yoyote itakayobashiri mechi hii na nyingine ambazo ni mali ya TFF itachukuliwa hatua kali za kisheria.

IMG_1075.jpeg
 
Mbona sijawahi kuona taarifa kama h kwenye mechi zngn za ligi na hua zipo kwenye ubashiri?
 
Mmmh!Hapa kuna upangaji wa matokeo kumbe kama makampuni ya betting hua yanauziwa haki hizo si vyepesi wao kuhonga team husika sasa.
 
Back
Top Bottom