TFF Wekeni Sheria, Tumechoka na wachambuzi waliokosa weledi wa soka hapa bongo

TFF Wekeni Sheria, Tumechoka na wachambuzi waliokosa weledi wa soka hapa bongo

mbingunikwetu

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2015
Posts
13,897
Reaction score
18,477
Tumechoka na wachambuzi maandazi wa soka hapa bongo!! Utakuta mtu hajaweahi hata kucheza mpira ligi yoyote, anatokea kuwa eti mchambuzi wa soka huku akiwakosoa marefarii waliosomea kazi yao.

Wengine wanadiriki hata kuwakosoa makocha wenye digrii zao!!! Wakome!! TFF chimbeni biti kali kuwa ni marufuku Redio yoyote kuruhusu mtangazaji wake kuchambua soka bila sifa hizo.

Pia iwe marufuku kwa kituo chochote cha luninga kuweka mchambuzi wa soka asiye na sifa. Hali kadhalika kwa vyombo vyote vya habari ikiwemo magazeti!

Mchambuzi wa kweli bongo hii ni Ally Mayai Tembele. Vituo vya TV viajiri wachambuaji wa kueleweka wenye heshima zao kwenye kandanda kama vile kina Sunday Manara, Abdallah Kibadeni, Zamoyoni Mogella, nk. Nawasilisha, karibuni wachangiaji kwenye uzi huu!
 
Kuna wengine tangu akiwa na umri wa miaka 5 hadi 50 ni shabiki mzuri.

Je, unataka kusema hawezi kuchambua kabumbu?
 
Kabisa maana wanazuia timu yetu kubebwa maana tukipewa penati wanasema tukibebwa kdg maneno mengi
Utakuwa shabiki wa makolo lazima hutak wachambue vile mbereko inafanya kazi
 
Kabisa maana wanazuia timu yetu kubebwa maana tukipewa penati wanasema tukibebwa kdg maneno mengi
Utakuwa shabiki wa makolo lazima hutak wachambue vile mbereko inafanya kazi
Makolo ndio mnyama gani?? mimi siko huko, mtu hajawahi kabisa kucheza soka la ushindani, atawezaje kuchambua mpira?
 
Kuna wengine tangu akiwa na umri wa miaka 5 hadi 50 ni shabiki mzuri.

Je, unataka kusema hawezi kuchambua kabumbu?
Aendelee kuwa mshabiki mzuri kama kina Kitenge, lakini kuchambua soka ni taaluma yenye wenyewe, awaachie kina Ally Mayai Tembele!!
 
Marufuku hii Kaitoa nani..!
Anyway Na mimi nakuunga mkono , Wengi wa wachambuzi wetu wa Sasa wanachambua huku wakiwa na Ushabiki wa usimba na Uyanga. Hili ndilo linalofanya kuwe na Ombwe la Uchambuzi yakinifu Kama ambavyo tulikuwa tunawaona kina
1. Mwl.Kashasha
2. Dr Ricky
3. Mwl.Tigana
Na Wengine wenye kariba ya hao niliowataja...
Sio Lazima sana kuwa ili Uwe Mchambuzi mzuri uwe ulikuwa 'unakipiga' . Lakini nadhani ni Muhimu ili uwe Mchambuzi Mzuri ni vizuri ufanye juhudi Kufuatilia Mpira na Historia yake Hapo ulipo na Ulimwenguni Kiujumla.Ujue Sheria zake. Sasa Hawa Wachambuzi wetu hata Historia tu Ya Soka la Tanzania hawajui.
 
Aendelee kuwa mshabiki mzuri kama kina Kitenge, lakini kuchambua soka ni taaluma yenye wenyewe, awaachie kina Ally Mayai Tembele!!
Hivyo hivyo na wao waendelee na kucheza mpira.

Kumbuka uchambuzi umesimama katika Taaluma na kipaji hivyo kuweka vigezo vyako hivyo siungi mkono.

Kuna wengine hawana ajira mbadala hivyo wanaishi kuilpitia uchambuzi na Kumbuka serikali inahamasisha kujiajiri.
Unazani watajiariji kwa kipi?

My take: Bora ushauri kuwa TFF iweke sheria kali kwa watakao fanya makosa katika uchambuzi.

Hitimisho: kwanza TFF wenyewe ni jipuuuui.
 
Nitajie mchambuzi yeyote Ulaya ambaye hajawahi kucheza soka katika ngazi za juu au kuwa kocha katika ngazi za juu!!! Acheni kujitoa ufahamu!
 
Back
Top Bottom