TFF ya shabiki na mwanachama wa Simba (Wallace Karia) imeanza kuibeba Yanga.?

demigod

JF-Expert Member
Joined
Jan 2, 2015
Posts
8,292
Reaction score
15,250
Habari humu.

Week iliyoisha imeshuhudia mabingwa watetezi, na timu kubwa na zenye historia kubwa ya kutwaa mataji kwenye Ligi zao wakitoa sare, haswa Mabingwa watetezi wakitoa sare kwenye michezo yao ya LigiKuu.

1. Real Madrid - Valencia
2. Dar Young Africans - Lipuli

Hizi zote zilishikwa shati na klabu za ligi huku zikiambulia sare.

Kwenye pambano ya Ligikuu Bara, mechi ya ufunguzi kati ya Yanga vs FCLipuli kulishuhudiwa moja ya Header safi kabisa iliyopigwa na Donald Ngoma ikimshinda mlinzi wa lango la FCLipuli na kugonga besela la juu na mwisho ukatua chini ikiwa ndani ya mstari wa golini.

Picha mbalimbali za marudio haswa ile ya karibu sana pale golini liyokuwa inaonyesha mahala ambapo mpira umedunda chini na hata kila mtu akaamini kuwa lilikuwa bao sahihi kwa kuwa hata wachezaji walio karibu walinyoosha mkono juu kuashiria ni bao halali.

Je, kutokea kwa minung'uniko kuwa lile halikuwa bao halisi kunathibitisha kuwa uongozi wa aliyekuwa shabiki na mwanachama wa Simba Bw Wallace Karia ameamua kuandaa m
waamuzi rasmi kwenye mechi za watani zake ili wawabebe watani zake kwa lengo lwa kuwasaidia wabebe ndoo kwa mara nyingine tena...?
 
Roho mbaya ni kitu kibaya sana, yaani wewe umeshinda goli 7 bila ila mwenzako kapata ka 1 tu ndio unaandika hapa upuuzi usio na kichwa wala miguu?
 
Roho mbaya ni kitu kibaya sana, yaani wewe umeshinda goli 7 bila ila mwenzako kapata ka 1 tu ndio unaandika hapa upuuzi usio na kichwa wala miguu?
Hajitambui huyo kindululu
 
Roho mbaya ni kitu kibaya sana, yaani wewe umeshinda goli 7 bila ila mwenzako kapata ka 1 tu ndio unaandika hapa upuuzi usio na kichwa wala miguu?

Ni mimi sijakuelewa wewe....au wewendio hunifahamu...?
 
Roho mbaya ni kitu kibaya sana, yaani wewe umeshinda goli 7 bila ila mwenzako kapata ka 1 tu ndio unaandika hapa upuuzi usio na kichwa wala miguu?
Ah...nadhani hujamuelewa vzr hyo anaitwa demigod mjangwani kabsaaaa huo uzi kauleta kimtindo flan hv utulie kumuelewa!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kulialia kwa sababu butu kiasi hicho. Mpira haukuvuka mstari wa goli
 
Na wewe ni among the great thinkers?

Povu tuwaachi wakina Diamond & Alikiba.

Je ni kweli shabikimwenzenu wa Simba (Karia) ameanza kuonyesha mahaba na Yanga au ni macho yangu yana makengeza.?
 
Acha kulialia kwa sababu butu kiasi hicho. Mpira haukuvuka mstari wa goli

Kwa hivyo tuna hitimishaje hili suala.?

maana kipindikileilikuwa Malinzi anaipendelea Yanga, Je leo tutakuwa tumekosea kusema shabiki/mwanachama ndakindaki wa Simba Rais wa TFF Bw W. Karia anaipendelea Yanga...?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…