Kufungwa kwa Starz kuna sababu nyingi..
- Morali ya timu naona imeshuka sana, siku hizi starz haina mvuto kabisa ikicheza hata hamu ya kutazama sina.
- Viwango vya wachezaji wetu, nao wengi wameshuka viwango, hawana ubora unaotakiwa kwenda nao kwenye timu ya taifa, huwa hawajitumi wameridhika sana.
Hapa sitaki kutupa lawama kwa TFF kwa kuruhusu wachezaji wengi toka nje, kwani hao wageni nao hufanya mazoezi yao pamoja na wazawa, mwisho wa siku kocha humpanga aliye bora, kocha hawezi kumpanga mzawa hata kama hana kiwango cha kuridhisha.
Uamuzi wa kumuondoa Kim naona ni sahihi, wacha apumzike mzee wa watu, mazingira aliyokutana nayo wakati huu sio sawa na yale ya wakati ule alipofanikiwa kutengeneza vijana wenye vipaji, leo mambo yamevurugika, wachezaji wengi wa sasa hawaeleweki, hata wanaocheza nje.
- Samatta kiwango kimeshuka.
- Msuva haeleweki.
- Ulimwengu haeleweki.