TFF yabadili ratiba, Azam vs Ndanda

TFF yabadili ratiba, Azam vs Ndanda

mkolaj

JF-Expert Member
Joined
Mar 24, 2014
Posts
3,023
Reaction score
1,089
Leo tena wamebadilisha ratiba ya mechi ya Azam vs Ndanda iliyobidi ipigwe hapo kesho tar 14.03.2015 Jumamosi badala yake mchezo huo umepelekwa mbele hadi tar. 16.03.2015 Jumatatu.

Viongozi wa timu zote mbili yaani Azam FC na Ndanda wanashangaa sababu za kubadili ratiba ya mechi yao.

TFF ni majanga!
 
Dah watu bana sasa hapo tff unatetewa kwa lipi,
Azam waliomba mechi yao ichezwa kesho na si jumapili kama ilivyokuwa imepangwa awali kwa kuwa siku hiyo kutakuwa na mchezo wa kimataifa wa Yanga,cha kushangaza tff wamewapeleka jpil
 
Kwani Ni Lini TFF Na Wakati Ule FAT Zilikuwa Na Heshima Ktk Nchi Hii au Taifa Hili? Heshima Kubwa Tutakayowapa Ni Mpaka Watufikishe Ktk Mafanikio Chanya Ya Kimpira Kwani Tumechoka Sasa Kugombania Timu Za Kushangilia Za Nchi Za Wenzetu Kila Kunapokuwa Na Mashindano Ya Either AFCON Or World Cup.
 
Yote hiyo ni kuihujumu Yanga tu. Yaani tunafungwa na Simba kwa sababu ya hujuma za TFF. Hapo juzi walimruhusu Ibrahimu Ajibu acheze mechi yetu dhidi ya Simba wakati ana kadi tatu za njano. Matokeo yake Ajibu akatoa pasi kwa Okwi ambaye akamfunga golikipa wetu Barthez, ambaye naye anatuhujumu.

TFF na Barthez, ni lini mtaacha kuihujumu Yanga? Hii ni hujuma, lazima tuende FIFA kudai pointi tatu
 
Ligi kuu ina timu 14 mpaka leo TUMEBADILI RATIBA MARA 13!Na bado,mpaka simba na yanga WAPATE NAFAS ZA MICHUANO YA KIMATAIFA MWAKANI ILI TUPATE PESA.
 
Hili ligi huwa akijisikia mtu yeyote anajipangia tu ratiba..
 
Hili ligi huwa akijisikia mtu yeyote anajipangia tu ratiba..
Kaburu amewakamata sana pale tff, yeye ndie anayefanya kaz ya kubadili badili ratiba bila kuwashirikisha wenzake,
Juzi kaimu mkurugenzi mkuu wa bodi ya ligi bi fatma anahojiwa na kituo cha redio cha magic fm kuhusu kubadili ratiba ya mechi ya mbeya city vs ruvu shooting anashangaa kuhusu mabadiliko ya ratiba ya mechi hiyo.
Sasa hapo ndipo panaposhangaza kama mkurugenzi wa bodi ya ligi hajui mabadiliko ya ratiba nani anaefanya kaz hiyo ya kubadili badili ratiba!!!!?
 
Kaburu kichwa, bila yeye wangeyumba zaidi.
 
Wacha uzushi wa kichawi wewe. Amri imetoka kwa Malinzi na Bodi imelalamika kuingiliwa na TFF. Jifunze kusema ukweli na fuatilia kwa watendaji wa TFF utapata ukweli. Wacha chuki binafsi na uzushi.
 
Back
Top Bottom