Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeliandikia barua Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (Caf) kuijulisha kuwa kuwa mechi ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Yanga dhidi Mamelodi Sundowans itachezwa kwa kufuata kanuni na taratibu za soka zilizowekwa.
Katika barua hiyo TFF imeihakikishia Caf kuwa mashabiki watapata fursa ya kuingia uwanjani kutazama mechi hiyo pasipo kulazimishwa kuonyesha hati ya kusafiria, kama ambavyo waziri wa utamaduni, sanaa na michezo, Damas Ndumbaro alisisitiza hivi karibuni.
“Ukija uwanja wa Taifa ukiwa umevaa jezi ya Mamelodi Sundowns lazima utuoneshe passport (hati ya kusafiria) ya Afrika Kusini na ukiwa na jezi ya Al Ahly utuoneshe passport ya Misri, nje na hapo ukifanya fujo Polisi watakuchukua ukapumzike kidogo utatoka baada ya mechi” alinukuliwa Damas Ndumbaro.
Hata hivyo katiba barua iliyoandikwa na TFF, imeijulisha kuwa taratibu zote za mpira wa miguu zitafuatwa katika mchezo huo na hakutokuwa na zuio lolote kwa mashabiki.
"Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linalihakikishia Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kuwa mechi husika itachezwa kwa kanuni na taratibu zilizowekwa za soka na namna ya utaratibu wa kuingia uwanjani.
"Kwa hivyo, sio kwamba pasipoti (pasi za kusafiria) zitatumika kama kigezo cha kuingia uwanjani kwa mashabiki wa Mamelodi Sundowns na mtu yeyote kwa sababu mechi ipo kikanuni na taratibu za mpira wa miguu bali sio kwa Idara ya Uhamiaji.
"Timu ya Mamelodi Sundowns imehakikishiwa usalama wao kutoka kwa vyombo husika wakati wote ambao watakuwa nchini na kuheshimu taratibu za mechi yao dhidi ya Young Africans SC, na Dhamana hii pia inawahusu maafisa wa mechi, mashabiki wa Sundowns wanaosafiri pamoja na mashabiki wanaoishi Tanzania na anaetaka kuhudhuria mechi hiyo," ilifafanua barua hiyo.
Kwahyo Kwa mujbu wa TFF sisi Mashabiki wa MAsandawana tunaoishi TZ tumeachwa huru kabisa