TFF yatoa tamko baada ya Shaffih Dauda kutangaza Ndondo Cup

TFF yatoa tamko baada ya Shaffih Dauda kutangaza Ndondo Cup

Smart codetz

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2023
Posts
218
Reaction score
875
Taarifa kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

7E64094E-C267-4470-92B8-378D770AD8D4.jpeg
 
Kwamba hayo mashindano hayana kibali miaka yote hiyo? Mwana Fa tusaidie hili NW
Inaana wao hawana akili hata waseme kuwa hayana kibali ilhai yanacho?Kama sheria inawataka waandaaji kuwa na kibali, kuna ubaya gani shirikisho kudai kibali?

Sheria zifuatwe sio kila siku watu binafsi waote mapembe ya kutaka kusumbuna na vyombo vilivyopo kisheria, huyo MWANA FA hawezi kusaidia ukiukwaji wa sheria.
 
Tff wana chuki binafsi na watu.

Mitaani kuna ndondo cup kibao...
Wewe binafsi umewahi kuandaa mashindano ya mpira bila kauwa na ridhaa yao (TFF).? Kama bado, kwanini unatoa reference ya vitu ambavyo hujui vinafanyikaje?

Nini dhima ya Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania (TFF), ikiwa yoyote anaweza kujifanyia atakalo kuhusu mpira?

NB: Kama huko nyuma TFF hawakuwa wanadai vibali basi walikuwa wanapwaya kimajukumu, na sio vibaya wao kuamua kusimamia sheria hivi sasa.

SHERIA ZIFUATWE.
 
Huu ni ukiritimba usio kuwa na tija yeyote.Kuandaa mashindano yasiyokuwa na affiliation na TFF uombe kibali.

Hawa wakinyamaziwa itakuwa hairuhusiwi hata kufanya mazoezi ya mpira bila kibali cha TFF.

Hakuna wanachoweza kufanya waendelee na Ndondo Cup tuone watafungia wangapi?

Hili likivumiliwa wataamua chochote wanachotaka.TFF wanataka pesa,kufungia wasema kweli badala ya kuendeleza mpira.Kuwanyima watu wasiandae mashindano ya mpira kunaendelezaje mpira?
 
Mashindano yangekua mapya nisingesema hivyo, mwaka wa 10 huu

Hata kama huko nyuma TFF walikuw hawaombi kibali, je sio jambo jema la kupongeza wao kuamua kusimamia utaratibu wa mashindano ya mpira kikamilifu hivi sasa?

Je wameomba kibali wakanyimwa?

Mimi ningeshangaa kama NDONDO CUP imeomba kibali kisha ikanyimwa.
 
Hatuna foundation nzuri ya mpira, kila siku tunahubiriwa mpira uchezwe ili vipaji vionekane,ila mchawi ni sisi wenyewe......Idd Nado alitoka ndondo cup -Mbeya City-Azam fc mpaka national team.......acha iendelee kunyesha tu......
 
Hata kama huko nyuma TFF walikuwaombi kibali, je sio jambo jema la kupongeza wao kuamua kusimamia utaratibu wa mashindano ya mpira kikamilifu hivi sasa?

Je wameomba kibali wakanyimwa?

Mimi ningeshangaa kama NDONDO CUP imeomba kibali kisha ikanyimwa.
Kwa nini iwe sasa wakati uzinduzi unakaribia? Kuna nakala yoyote ya kuwa kila mashindano lazima yawe na kibali iliyotoka kabla ya barua ya leo?
 
Hata kama huko nyuma TFF walikuwaombi kibali, je sio jambo jema la kupongeza wao kuamua kusimamia utaratibu wa mashindano ya mpira kikamilifu hivi sasa?

Je wameomba kibali wakanyimwa?

Mimi ningeshangaa kama NDONDO CUP imeomba kibali kisha ikanyimwa.
Wanaugomvi binafsi na mwajiriwa wa taasisi ambayo ni clouds ,ni ujinga yale siyo mashindano ya Shafii ila alikuwa mmoja wa waratibu na saizi anaratibu Mkazuzu
 
Tff wana chuki binafsi na watu.

Mitaani kuna ndondo cup kibao.

Kuna diwani cup

Kuna mbunge cup.

Kuna kombe la mbuzi, ng'ombe na majogoo

Je vibali wanatoa TFF ?
Bifu lao tu Ndimbo na Dauda wanavimbiana na Startimes TV3 si ndio wanarushaga ndondo cup au imekuaje?
 
Kwa nini iwe sasa wakati uzinduzi unakaribia? Kuna nakala yoyote ya kuwa kila mashindano lazima yawe na kibali iliyotoka kabla ya barua ya leo?

Kwamba muda wa kuomba kibali umeisha kwakua tangazo limetoka leo?

Wao waombe kibali mashindano yaendelee, hizi habari za kila mtu kutaka huruma za wananchi ili sheria zipindishwe kwa masilahi yake binafsi ni ushamba. Alianza Manara kutafuta huruma sasa ni DAUDA, mwisho wa siku sheria ni lazima zifuatwe.
 
Back
Top Bottom